August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Katiba mbovu inaibeba serikali’

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari. Kulia ni Ofisa Mipango wa Jinsia na Watoto wa LHRC, Naemy Sillary

Spread the love

KATIBA ya Tanzania ni mbovu. Hali hiyo imekuwa ikitumiwa na serikali kufanya uamuzi wenye msukumo wa kichama zaidi, anaandika Faki Sosi.

Harold Sungusia, Wakili na Mwanaharakati wa Haki za Binaadamu Tanzania amesema kuwa, zuio la mikutano ya vyama vya siasa nchini lililotolewa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) linatokana na kutokuwa na Katiba nzuri.

Akizungumza na MwanaHALISI Online amesema, hatamu ya nchi imeshikwa na chama tawala pekee na kwamba, wamekuwa wakiongoza kwa utashi wao wa kisiasa.

Sungusia ametoa mfano kwamba, Mwenyekiti wa Usalama wa Wilaya ni Mkuu wa Wilaya ambaye ni kada wa CCM na kuwa, Mkuu wa Polisi Wilaya huwa chini kada huyo.

“Je, umewahi kusikia chama tawala kimenyimwa kibali cha kufanya mikutano yao pale kinapoamua?” amehoji Sungusia.

Amesema kuwa, kutokana Katiba yetu, rais aliyepo madarakani ndiye anayeteuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) na makameshna wengine wa tume ambao hutokana na itikadi yake.

“Angalia mazingira haya, rais anayetokana na chama cha siasa ndiye anayeteua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi.

“Hawezi kumteua mtu ambaye hawafanani itikadi, sasa katika mazingira haya unategemea nini wakati wa uchaguzi?” amehoji.

 

error: Content is protected !!