Friday , 1 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kata 43 kuamua madiwani wao, mawakala wa Chadema wazuiwa
Habari za SiasaTangulizi

Kata 43 kuamua madiwani wao, mawakala wa Chadema wazuiwa

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Semistocles Kaijage
Spread the love

UCHAGUZI mdogo wa udiwani katika kata 43 zilizoko kwenye halmashauri 36 za mikoa 19 ya Tanzania Bara unafanyika leo, huku kukiwa na malalmiko kibao, anaandika Mwandishi Wetu.

Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), uchaguzi huo unafanyika kutokana na sababu kadhaa, zikiwemo madiwani kufariki dunia, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na wengine ushindi wao kutenguliwa na mahakama.

Mkoa wa Arusha unaongoza kwa kuwa na kata nane miongoni mwa hizo ni za madiwani waliojiuzulu kutoka Chadema na kuhamia CCM wakieleza ni kutokana na kumuunga mkono Rais John Magufuli.

Arusha ambapo kumekuwa na mtikiso mkubwa kwani baadhi ya maeneo mawakala wa Chadema wanalalmika kukatazwa kuingia kwenye vituo.

Uchaguzi huu ni wa pili tangu kuanza mwaka huu. NEC katika taarifa yake imesema inatakiwa kufanya uchaguzi wa madiwani mara mbili kwa mwaka kwa mujibu wa sheria. Uchaguzi mdogo mwingine wa ubunge na udiwani ulifanyika Januari 22 mwaka huu.

Ratiba ya mchakato wa uchaguzi huo ilianza Oktoba 26 kwa vyama vya siasa kufanya uteuzi wa wagombea wa udiwani na kampeni zilianza Oktoba 27 na kuhitimishwa jana.

NEC katika taarifa kwa vyombo vya habari jana imevitaka vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi kuhakikisha unafanyika kwa amani na utulivu na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage amesema wapiga kura wapatao 333,309 wanatarajiwa kupiga kura katika vituo 884 ambako walijiandikishia kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2015.

Amesema tofauti na chaguzi zilizopita, NEC kwa kuzingatia masharti ya Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa kifungu cha 62 imewaruhusu wapiga kura ambao ama kadi zao za kupigia kura zimepotea, kuchakaa au kufutika kutumia vitambulisho mbadala kwenda katika vituo walivyojiandikisha ili waweze kupiga kura katika uchaguzi huu.

Jaji Kaijage amesisitiza ili kuruhusiwa kutumia kitambulisho mbadala, sharti majina ya mpiga kura yafanane kwa herufi na majina yaliyoko katika kitambulisho mbadala ambayo yako katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Vitambulisho mbadala ambavyo NEC imeruhusu vitumiwe na wapiga kura ni leseni ya udereva, kitambulisho cha uraia kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) na pasi ya kusafiria.

Pia, amewataka wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoa kipaumbele kwa makundi maalumu wakati wa kupiga kura, ambayo ni ya walemavu, wajawazito, wenye watoto wachanga, wazee na wagonjwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Rais Mwinyi kuzikwa Machi 2 visiwani Unguja

Spread the loveMWILI wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania,...

Habari za SiasaTangulizi

Rais mstaafu Mwinyi afariki dunia

Spread the loveRais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan...

Habari za Siasa

Waziri mkuu Ethiopia atua Tanzania

Spread the loveWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia,...

Habari za Siasa

Babu Owino: Vijana msibaki nyuma

Spread the loveMbunge wa Embakasi Mashariki nchini Kenya, Paul Ongili Owino maarafu...

error: Content is protected !!