January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kasulumbayi: Serikali imeishiwa mbinu

Mbunge wa Maswa Mashariki (CHADEMA) Sylvester Kasulumbai

Spread the love

MBUNGE wa Maswa Mashariki, Slyvester Kasulumbayi (Chadema) amesema, serikali imeishiwa mbinu katika kubuni vyanzo vipya vya mapato. Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na MwanaHALISIonline baada ya kupitishwa Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2015/16.

Mbunge huyo amesema, kama serikali ingekuwa na ubunifu ingeweza kukusanya mapato mengi kupitia sekta ya mifugo na uvuvi.

“Kuna vyanzo vingi vya mapato ambavyo serikali imekuwa ikividharau na badala yake wamekuwa na akili ya kukariri vyanzo vile vile miaka yote.

“Tanzania ni nchi ya tatu Afrika kwa kuwa na mifugo mingi na kama serikali ingekuwa na ubunifu wa kuweka miundombinu sahihi kwa wafugaji, ni wazi wangepata kipatato kubwa,” amesema Kasulumbayi.

Amesema, inasikitisha kuona serikali inasema mifugo kama vile ng’ombe ni waharibifu wa mazingira wakati ni rasilimali ambayo haihitaji kuwa na utafiti.

“Jambo lingine ambalo serikali inashindwa kutambua ni pale ambapo wanataka wafugaji kupunguza mifugo yao wakati hakuna miundombinu yoyote ambayo itawasaidia pale watakapokuwa wameuza mifugo hiyo.

“Ng’ombe siyo mnyama mharibifu kama inavyosemwa na viongozi wa serikali, hata katika vitabu vitakatifu inaonesha wazi kuwa mnyama huyo ni mpatanishi.

“Serikali imeshindwa kutambua kuwa mnyama huyo ni rasilimali kubwa kwani kila sehemu ya mnyama huyo ni mali,” amesema.

Akizungumzia malisho Kasulumbayi amesema, serikali imeshindwa kutenga maeneo kwa ajili ya kulishia mifugo.

Akielezea sekta ya uvuvi amesema, Tanzania inakosa mapato mengi kutoka katika maziwa na bahari kutokana na viongozi ndani ya serikali kutokuwa na wabunifu.

error: Content is protected !!