Sunday , 2 April 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kasubi ataja vipaumbele akichaguliwa Mzimuni
Habari za Siasa

Kasubi ataja vipaumbele akichaguliwa Mzimuni

Spread the love

BAKAR Kasubi, mgombea Udiwani wa Mzimuni Kinondoni, jijini Dar es  Salaam amawaeleza wananchi wa kata hiyo endapo watamchagua atahakikisha wananchi wanapata asilimia 10 ya mapato ya eneo hilo kama sehemu ya mikopo yao, Anaripori Faki Sosi, Dar es Salaa  … (endelea).

Sera hizo amezinadi jana Jumapili tarehe 20 Septemba 2020 kwenye viwanja vya Mtambani wakati akizindua Mikutano ya kampeni zake.

“Kipaumbele changu cha kwanza ni kuhakikisha asilimia kumi ya mapato ya Kata Mzimuni inayaokwenda Halmashauri itarudi kwetu kama mikopo…kwa sababu changamoto yetu kubwa ni umasikini.”

“Mkopo ni jambo la lazima na la kisheria kwa sababu sote tunalipa kodi na kisheria asilimia kumi inatakiwa irudi kwetu”

Kasubi amesema, Zahanati ya Mzimuni atahakikisha inafanya kazi saa 24 na kwamba haitakuwa kama sasa inafunguliwa saa mbili asubuhi na kufungwa saa kumi na mbili jioni.

Amesema, atasimamia ujenzi wa ukuta wa shele ya msingi ya Mzimuni pia kuhakikisha shule ya kata hiyo kuwa na maabara kwa ajili ya kufundishia masomo ya Sayansi.

Kuhusu kipaumbele chake cha tatu amesema, akipewa ridhaa ya kuwa Diwani atahakikisha mitaro inayopitisha maji taka itazibuliwa ili kuondoa adha ya mafuriko kwa wananchi.

Kuhusu suala la tozo ya ulinzi inayotozwa isivyohalali atahakikisha tozo hiyo inatolewa kihalali.

Kasubi amesema, kwenye kata hiyo ni kero ya takataka na kwamba zinapelekea kuziba mitaro ya kupitishia maji  atahakikisha Halmashauri inasimamia zoezi hilo.

Kipaumbele cha mwisho, Kasubi amesema akichaguliwa kuwa diwani wa kata hiyo atafufua time zote za mpira zilizokufa kwenye kata hiyo kwa kuhakikisha uwanja wa mpira wa mzimuni unarejeshwa kwa wananchi.

Hapa Mzimuni tumetoa wachezaji wanaocheza ligi kuu kwa sababu ya uwanja ule hivyo tutahakikisha unarudishwa kwa wananchi wa Mzimuni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia apangua mawaziri

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la...

Habari za Siasa

RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia

Spread the loveALIYEWAHI kuwa mkuu wa mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na...

Habari za Siasa

Marekani kuwekeza Dola 500 Mil kupeleka bidhaa na huduma Tanzania

Spread the loveMAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema miongoni mwa...

Habari za Siasa

Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani

Spread the loveKATIKA kuimaridha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania...

error: Content is protected !!