September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kasi ya Corona yamshtua JPM, atangaza siku 3 za maombi

Spread the love

RAIS John Magufuli ametaka Watanzania kumuomba Mungu kwa siku tatu mfululizo, ili awanusuru na athari za Ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu, inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mkuu huyo wa nchi ametoa wito huo leo tarehe 16 Aprili 2020, kupitia ukurasa wake wa Twitter, kipindi ambacho kasi ya ueneaji wa ugonjwa huo imeongezeka,  ambapo kwa sasa Tanzania ina wagonjwa 94 wa COVID-19.

Rais Magufuli amewataka Watanzania kufanya maombi kila mmoja kwa imani yake, kuanzia kesho tarehe 17 hadi 19 Aprili mwaka huu.

“Ndugu zangu Watanzania, kutokana na ugonjwa wa Corona, nawaomba tutumie siku 3 za kuanzia tarehe 17- 19 Aprili, 2020 (Ijumaa, Jumamosi na Jumapili) kumuomba Mwenyezi Mungu aliye muweza wa yote, atuepushe na janga la ugonjwa huu. Tusali kwa kila mmoja kwa imani yake, atatusikia,” ameandika Rais Magufuli.

Jana wizara ya afya iliripoti wagonjwa wapya 29 na kufanya idadi ya wagonjwa hao kuwa 88. Leo wizara ya afya Zanzibar imeripoti wagonjwa wapya 6 na kufikisha idadi ya wagonjwa 94.

error: Content is protected !!