Tuesday , 30 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kashfa za serikali zalikwaza Bunge
Habari za Siasa

Kashfa za serikali zalikwaza Bunge

Spread the love

BUNGE la Tanzania limeonesha kutoridhishwa na namna serikali inavyotekeleza wajibu wake wa kupeleka fedha za miradi kama ambavyo inapaswa kuwa.Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma…(endelea).

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) leo tarehe 2 Januari 2019 imewasilisha taarifa yake huku ikiibua kashfa kadhaa kuhusu uendeshaji wa taasisi za umma.

Moja ya masuala muhimu yanayotajwa kama tatizo kubwa ni kushindwa kwa serikali kutoa fedha kwa wakati kwa ajili ya kuwezesha mashirika na taasisi zake kujiendesha.

Kamati ya Bunge imeikosoa serikali kwa mtindo wake wa kutopeleka kwa wakati mafungu ya fedha hata pale inapokuwa imepata migao yake kutokana na shughuli zinazofanywa na mashirika na taasisi zilizo chini ya serikali.

Imeelezwa kuwa, tabia hiyo imekuwa ni kikwazo cha ufanisi kwenye taasisi na mashirika ya serikali.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji kazi za kamati hiyo kwa mwaka uliopita,mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Raphael Chegeni amesema, pamoja na serikali kufufua baadhi ya mashirika yake na kuongeza chachua sekta nyingi za kiuchimi, uchambuzi wa kamati umebaini kuwa bado kuna changamoto ya ukosefu wa mitaji kwa baadhi ya taasisi na mashitika ya umma.

Taasisi zenye upungufu wa mtaji ni pamoja na benki ya posta Tanzania, Benki ya Maendeleo ya Kilimo, Shirika la Mawasiliano Tanzania, Kampuni ya Huduma za Meli pamoja na Benki ya Maendeleo (TIB) ,” amefafanua.

Katika upungufu huo, kamati imebaini kuwa serikali inatakiwa kuongeza mitaji katika Shirika la Mawasiliano la Taifa ili liweze kufanya kazi zake kwa ufanisi na kuendana na kasi ya ushindani.

Kamati iimeeleza kuwa, katika uchambuzi uliofanywa kwenye Shirikaka la Mawasiliano Tanzania (TTCL) umeonesha kuwa madeni ambayo shirika linazidai taasisi mbalimbali yameongezeka kutoka Sh.bilion 106.4 mwaka 2015/16 hadi kufikia Sh. bilion 155.6 mwaka 2016/17 ikiwa ongezeko la asilimia 46.2.

“Bado kuna upungufu mkubwa wa mtaji ili shirika liweze kukabiliana na ushindani uliopo katika sekta ya mawasiliano kwa kuwa sekta hiyo inakiwa kwa kasi.“Mpango wa biashara wa TTCL unaeleza kuwa kampuni inahitaji jumla ya Dola za Marekani 762 katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2019/20hadi 2022/23” amefafanua.

Mbali na hayo kamati imebaini kuwa, taasisi za umma zimeshindwa kutekeleza sera na miongozo ya Ushiriki wa Sekta Binafsi na Sekta za Umma (PPP) katika kuendesha miradi.

Kutokana na hali hiyo kamati ya utekelezaji wa mitaji ya umma imekuwa ikiangalia utekelezaji wa miradi ya uwekezaji wa kibiashara.

“Hata hivyo changamoto hiyo inaweza kutatuliwa iwapo taasisi za serikali zitaingia ubia na sekta binafsi (PPP)katika utekelezaji wa miradi mbalimbali,” amesema Dk. Chegeni.

Kamati hiyo inependekeza ambayo ni taasisi na mashirika ya umma kutakiwa kuwa na mtazamo wa kibiashara ili yaweze kutumika kikamilifu rasilimali walizonazo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

Habari za Siasa

ACT Wazalendo yaanika madudu miradi ya ujenzi, moundombinu

Spread the loveCHAMA cha ACT Wazalendo kimeeleza wasiwasi juu ya uelekeo wa...

Habari za Siasa

Samia ashuhudia utiaji saini ujenzi wa minara 758 ya bilioni 265

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa kampuni za...

error: Content is protected !!