Sunday , 29 January 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Kashfa ya ufisadi yaitafuna Ukraine katikati ya vita
Kimataifa

Kashfa ya ufisadi yaitafuna Ukraine katikati ya vita

Spread the love

 

RAIS wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy amesema anafanya mabadiliko ya maafisa wake wa ngazi ya juu na chini serikalini, kutokana na madai ya ufisadi yaliyoibuka nchini humo tangu Urusi iivamie nchi yake Februari mwaka jana. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Sakata hilo la ufisadi huenda likapunguza ari ya nchi za Magharibi kuisaidia serikali yake wakati ambapo kuna mvutano miongoni mwa mataifa ya Ulaya kuhusu suala la kupeleka vifaru chapa Leopard 2 kutoka Ujerumani kueleke Ukraine.

Ukraine inasema inavihitaji vifaru hivyo ili kukabiliana na jeshi la Urusi na kuyarudisha katika himaya yake maeneo yaliyotekwa.

Juzi tarehe 22 Januari, 2023, polisi wa kukabiliana na ufisadi nchini Ukraine walisema kwamba wanamshikilia naibu waziri wa miundombinu kwa madai ya kupokea rushwa ya dola 400,000 katika uagizaji wa jenereta kutoka nje ya nchi mwezi Septemba.

Utafiti mmoja wa gazeti pia uliituhumu wizara ya ulinzi kwa kulipa fedha kupita kiasi kwa ajili ya chakula cha wanajeshi. Ukraine ina historia ndefu ya ufisadi na utawala usio thabiti.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

DCI ajitosa uchunguzi matokeo uchaguzi mkuu Kenya

Spread the loveOFISI ya Mkurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)...

HabariKimataifa

Aliyesomeshwa na mchumba aamuriwa kurudisha Sh 9.4 Mil. baada ya kukataa kuolewa

Spread the love  MWANAMKE mmoja nchini Uganda ambaye aliuumiza moyo wa mchumba...

Kimataifa

Uganda yaanza kuchimba mafuta

Spread the love  UCHIMBAJI wa kwanza wa mafuta kibiashara nchini Uganda umeanza...

Kimataifa

Afrika kusini waandamana kushinikiza serikali kumaliza tatizo la umeme

Spread the love  MAMIA ya wafuasi wa Chama cha upinzani nchini Afrika...

error: Content is protected !!