Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kashfa ya kununuliwa CCM yamtesa Mbowe, ‘mwenye ushahidi ajitokeze’,
Habari za SiasaTangulizi

Kashfa ya kununuliwa CCM yamtesa Mbowe, ‘mwenye ushahidi ajitokeze’,

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe leo Jumamosi amesema kashfa ya kutuhumiwa kuwa amekula rushwa au amelamba asali ili kushiriki maridhiano ya kitaifa na CCM ni mojawapo ya kashfa mbaya zilizopitiliza na kushusha heshima yake kwa jamii katika kipindi cha miaka 30 aliyoitumikia Chadema. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza … (endelea).

Pia ametoa wito kwa mwanachama au mtu yeyote mwenye ushahidi kwamba amechukua senti tano ya CCM ili ashiriki maridhiano hayo ya kitaifa ajitokeze.

Mbowe ametoa kauli hiyo leo tarehe 21 Januari, 2023 wakati akihutubia mamia ya wafuasi wa Chadema na wananchi waliojitokeza katika uzinduzi rasmi wa mikutano ya hadhara ya chama hicho kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.

Amesema baadhi ya Wana-Chadema walijengewa hofu kwamba mwenyekiti wao ameuzwa kashfa ambayo ni mbaya katika kipindi chote cha miaka 30 kwenye utumishi waka Chadema.

“Anasimama kiongozi wa chama changu anasema Mbowe amepewa asali! nimepoteza mabilioni ya fedha kwenye chama hiki… nimeitesa familia, wanakuja wenzangu wanaotakiwa kuniunga mkono wanasema nimekula rushwa?

“Kwangu ni insult (kashfa) iliyopitiliza, yeyote mwenye ushahidi kwamba Mbowe nimekula senti tano ya mtu asimame aseme… kwa sababu mnaua heshima yangu.

“Mambo ya kuumizana, kudhalilishana siwezi kuyakubali, lakini leo tukubaliane, tusamehe ya nyuma tuende mbele na kwa hilo niko tayari,” amesema Mbowe.

Amesema jambo hilo limemuumiza sio yeye pekee bali pia,watoto wake na mke wake kwa sababu wanajua amepoteza mabilioni mangapi lakini anatokea kiongozi wa Chadema anasema amekula asali na kuaminisha umma.

“Kwa namna amabvyo viongozi wangu wameteswa na kuumiwa upande wa pili wana haki ya kuwa na hisia hizo. Lakini niwaombe viongozi wangu tuna wajibu mkubwa katika nchi yetu,” amesema.

1 Comment

  • Mimi siyo mkereketwa ktk siasa lakini ktk hili inanibidi. Mh Mbowe pole sana. Kmbuka MAMLUKI ktk siasa ndiyo kwao na hasa TZ, wengine wanawania nafasi Yoko kihivyo. Hiyo mabomu siyo ya kupuuzia, wenzetu wemewania kutawala milele lakini wakumbuke ni Mungu tu ndiye milele yote na CCM wasitupotoshe. Baada ya Mw Nyerere ni wewe pekee mpigania haki wa kweli wengine wanakamia kujaza matumbo tu. Watanzania tuna wajibu wa kukuombea na kukupigania ktk kutuongoza kwa usawa na
    haki kwani wengine ndiyo walewale. Tunaendelea kukuombea kwa Mungu uweze kutimiza hayo na mengine unayoagizwa na Mungu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!