Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kasesela, Odunga, Ole Sabaya watemwa U DC
Habari za Siasa

Kasesela, Odunga, Ole Sabaya watemwa U DC

Lengai ole Sabaya
Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa wakuu wa wilaya (DC) 139 katika mikoa ya Tanzania Bara. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Uteuzi huo, umefanyika jana Jumamosi, tarehe 19 Juni 2021 huku ukishuhudia Rais Samia akiwaweka kando baadhi yao wakiwemo, Richard Kassela wa Iringa na Simon Odunga wa Rorya mkoa wa Mara.

Mwingine ni Lengai Ole Sabaya ambaye huyu alimsimamisha tarehe 13 Mei 2021, kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Lengai ole Sabaya

Tayari vyombo vimekwisha mpandisha mahakamani yeye pamoja na wezake watano kwa mashtaka sita ikiwemo, rushwa, uhujumu uchumi, unyang’anyi wa kutumia silaha na kuongoza genge la uhalifu.

Kesi yake inaendelea mahakama ya Arusha na tayari nafasi yake ameteuliwa, Juma Irando.

Ingawa Rais Samia hajaelezea sababu za kuwaweka kando, Odunga na Kasesela, lakini Odunga amekuwa akilalamikiwa na wananchi anaowaongoza kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela

Kwa upande wa Kasesela, ambaye amehudumu kwa zaidi ya miaka mitano Wilaya ya Iringa, katika miezi ya karibuni, kulisambaa ‘clip’ ya video mitandaoni, akizozana na wananchi.

Katika video hiyo, inamwonyesha Kasesela akimtolea lugha isiyo na staha mwananchi kwenye moja ya mgogoro wilaya humo, hali iliyomfanya kuomba radhi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!