Tuesday , 5 December 2023
Home Kitengo Michezo Karia ruksa kuwania uongozi FIFA
Michezo

Karia ruksa kuwania uongozi FIFA

Walace Karia, Rais wa TFF
Spread the love

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imeidhinisha kuwa rais wa sasa wa shirikisho hilo, Wallace Karia kugombea ujumbe wa baraza ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa nchi zinazungumza lugha ya kingereza kwenye uchaguzi unaotarajia kufanyika mwezi machi, mwakani. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kamati hiyo ambayo ilikutana mkoani Tanga hivi karibuni katika vikao vyake vya kawaida, kilipitia taarifa mbalimbali za utekelezaji kwa kipindi cha miezi mitatu na kupitisha maadhimio mbalimbali.

Uchaguzi huo wa Fifa utatoa nafasi mbili kwenye kinyang’anyiro cha ujumbe wa baraza kuu kwa nchi hizo zinazo zungumza lugha ya kingereza kama ilivyo kwa mujibu wa kanuni.

Tarifa kutoka ndani ya TFF zimeeleza kuwa wajumbe wa mkutano huo waliridhia kwa ujumla wao na kumruhusu Karia kuingia katika kinyang’anyiro hiko ndani ya Fifa.

Aidha maadhimio mengine yaliyofikiwa kwenye kikao hiko ni pamoja kumteua, Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi wa Idara mpya ya Sheria, Habari na Masoko mara baada ya kuziunganisha ili kuleta ufanisi wa kiutendaji.

Kabla ya uamuzi huo, idara hizo tatu kila moja ilikuwa inajitegemea katika utendaji kazi wake ndani ya TFF mpaka yalipofikiwa maamuzi hayo.

Boniface Wambura, Mkurugenzi wa Idara mpya ya Sheria, Habari na Masoko

Pia kamati hiyo imepitia mpango wa TFF wa kuanzisha shule ya uongozi wa mpira wa miguu ili kukabili changamoto za uongozi kwenye taasisi za mpira wa miguu ambao utawahusisha baadi ya wataalam kutoa vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini.

Katika hatua ya nyingine kamati tendaji ya TFF ilipokea na kupitia taarifa mbalimbali za miradi ya kimaendeleo kwa mikoa ya Dare es Salaam na Tanga ambapo hivi karibuni shirikisho hilo itasaini makubaliano ya mkandarasi aliyeshinda tenda hiyo.

Kamati hiyo pia imepanga tarehe ya kufanyika mkutano mkuu wa mwaka wa TFF, ambao umepangwa kufanyika mkoani Kigoma 19, Desemba, 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaMichezo

Mwana FA anogesha Tamasha la Exim Bima Festival

Spread the loveNAIBU Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana...

Michezo

Manchester City dhidi ya Tottenham ni usiku wa kisasi

Spread the love KIPUTE kati ya klabu ya Manchester City dhidi yaTottenham Hotspurs...

Michezo

Wikiendi ya kutamba na Meridianbet hii hapa usikubali kuikosa

Spread the loveMERIDIANBET wanakwenda kukupa nafasi ya kutambawikiendi hii kupitia ODDS KUBWA walizoweka...

Michezo

Fernandes hakamatiki Man Utd, mahesabu ni kuifunga Bayern

Spread the love  NAHODHA wa Manchester United, Bruno Fernandes, alikuwa na kiwango...

error: Content is protected !!