May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Karia athibitishwa Rais TFF

Wallace Karia, Rais wa TFF

Spread the love

 

WAJUMBE wa mkutano mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wamemuthibitisha Wallace Karia kuendelea kuwa Rais wa shirikisho hilo kwa muhula wa pili wa miaka minne. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga … (endelea).

Karia alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo ya urais katika uchaguzi huo, unaofanyika leo Jumamosi, tarehe 7 Agosti 2021, jijini Tanga. Wajumbe hao wamepiga kura ya wazi.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi huo, Wakili Kilomoni Kibamba amewahoji wajumbe wa mkutano huo wanaompinga Karia hakuna aliyesimama.

Wakili Kilomoni amesema, wajumbe halali ni 80 ambao wote wamemthibitisha Karia kuendelea kuwa Rais wa TFF sawa na asilimia 100.

error: Content is protected !!