May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Karia afunguka sababu za kuarishwa mechi ya Simba na Yanga

Walace Karia, Rais wa TFF

Spread the love

 

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), amesema sababu za kiusalama ndiyo zilipelekea kuarishwa kwa mchezo kati ya Simba na Yanga uliotakiwa kuchezwa tarehe 8 Mei, 2021, kwenye Uwanja wa Benjamin Mpaka, Dar es Salaam. Anaripoti Kelvini Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, namba 208, uliharishwa baada ya klabu ya Yanga kugomea mabadiliko ya muda yaliofanywa na TFF walipokea maelekezo kutoka wizarani kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ya kuwa mchezo huo uchezwe saa 1 usiku badala ya saa 11 jioni kama ilivyokuwa hapo awali.

Karia amefunguka hayo kupitia mahojiano yake na TFF TV, katika kipindi chao kinachoruka hewani Azam TV na kueleza kuwa bodi ya Ligi walikuwa na jukumu la kueleza sababu za kuahirishwa kwa mchezo huo na walifanya hivyo kwa kuanisha kanuni mbalimbali na kisha kueleza kuwa sababu za kiusalama ndizo zilizolekea mchezo huo kuota mbawa.

“Kuna sehemu tulinukuliwa kuwa Rais hajui sababu za kuahirishwa kwa mchezo, ni kweli kikanuni sikuwa msemaji wa bodi ya Ligi, ila wao bodi wanaweza kutoa sababu za kuahirishwa na ilifanya hivyo kwa kuanisha kanuni ambazo zinaeleza ikitokea jambo gani, mchezo unaweza kuhairishwa, hasa sababu kubwa ilikuwa za kiusalama,” alisema Karia.

Aidha Karia aliongezea kuwa, wao kama TFF wanamaamuzi ambayo kikanuni hayawezi kuingiliwa na mtu mwingine, lakini alidai kuwa huu mpira hawachezi peke yao, bali wanashirikiana na serikali kwa kuwa hata kwenye vikao vya mechi wanashiriki.

Tayari Wizara imeshatoa tamko kuitaka TFF, kupanga upya tarehe ya kuchezwa kwa mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kurejesha pesa kwenye kadi ambazo mashabiki walitumia kuingia Uwanjani kutazama mchezo huo ambao kiuhalisia hakufanyika.

error: Content is protected !!