Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Karantini ya Covid kwa wasafiri China mwisho Januari
Kimataifa

Karantini ya Covid kwa wasafiri China mwisho Januari

Spread the love

 

CHINA itaondoa karantini kwa wasafiri kuanzia tarehe 8 Januari, maafisa wamesema, kuashiria mabadiliko makubwa ya mwisho kutoka kwa sera ya sifuri ya Uvik0-19 ya nchi hiyo. Yanaripoti Mashirika ya Kimataifa … (endelea)

Baada ya miaka mitatu ya mipaka iliyofungwa, hii itafungua tena nchi kwa wale walio na safari za kazi na kusoma, au wanaotaka kutembelea familia.

Hatua hii inakuja wakati ambao China inapambana na kuenea kwa virusi hivyo kwa sababu ya vizuizi kuondolewa.

Ripoti zinasema hospitali zimezidiwa na wazee wanakufa.

Idadi ya kweli – hesabu za kila siku na vifo – haijulikani kwa sasa kwa sababu maafisa wameacha kutoa takwimu ya Covid.

Beijing ilikuwa imeripoti takriban maambukizo mapya 4,000 ya Covid kila siku wiki iliyopita na vifo vichache.

Siku ya Jumapili ilisema itaacha kuchapisha nambari za kesi kabisa.

Lakini kampuni ya takwimu ya afya ya Uingereza Airfinity ilikadiria China ilikuwa ikipata maambukizi zaidi ya milioni moja na vifo 5,000 kwa siku, kulingana na Reuters.

Sera inayoitwa “zero-Covid” ilidhoofisha uchumi na kuwafanya raia kuchoka kwa vizuizi na vipimo vya mara kwa mara.

Chuki dhidi ya sera hiyo ililipuka na kwa kufanyika maandamano adimu ya umma dhidi ya Rais Xi Jinping mnamo Novemba, ambayo yalisababisha viongozi kutupilia mbali sheria za Covid wiki chache baadaye.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Ramaphosa akiri tatizo la umeme Afrika Kusini kuathiri sekta ya madini

Spread the love  RAIS wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema tatizo la...

Kimataifa

Idadi ya vifo tetemeko la ardhi yafikia 9000

Spread the love  IDADI ya vifo vilivyotokana na tetemeko la ardhi lililotokea...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi Uturuki: Vifo vyaongezeka hadi 4,800

Spread the love  Idadi ya vifo vilivyotokana na tetemeko lililotokea jana Jumatatu...

Kimataifa

Tetemeko la ardhi laua watu 300 Uturuki, Syria

Spread the love  WATU  300 wamefariki dunia katika tetemeko kubwa la ardhi...

error: Content is protected !!