July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kapuya amchongea Mkuu wa Wilaya

MBUNGE wa Urambo Magharibi, Prof. Juma Kapuya

Spread the love

MBUNGE wa Urambo Magharibi, Prof. Juma Kapuya (CCM) ametaka ufanyike uchunguzi yakinifu juu ya matumizi ya Sh. 500 milioni katika Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora. Anaandika Hosea Joseph, Kaliua (endelea).

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara juzi jimboni humo, Prof.  Kapuya amesema ana wasiwasi juu ya matumizi ya fedha hizo zilizotolewa kwa ajili ya ununuzi wa changarawe za ujenzi wa barabara katika wilaya hiyo.

Amesema kutokana na uongozi usioridhisha wa Mkuu wa Wilaya aliyepia, Saveli Maketa, hana imani juu ya matumizi ya fedha hizo zilizotolewa ili kuwasaidia wanyonge.

“Nikuombe Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi mjitahidi kulishughulikia suala
hili na kuita ukaguzi wa hesabu ya matumizi ya fedha hizo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa ikiwa kuna ubadhirifu wowote,” amesema.

Katika hatua nyingine, Prof. Kapuya, alitumia fursa hiyo kumkaribisha mkuu mpya wa wilaya, Venance Mwamoto na kuwataka wananchi wa Kaliua kumpa ushirikiano.

“Nakuomba uwe mkuu wa wilaya wa vyama vyote, dini zote na watu wote maana aliyepita hatujui alikuwa wa aina gani. Wananchi hawakuwa na ushirikiano naye kwani amewahi kuzuia hata wanakwaya kuimba jirani kwamba wanampigia kelele,”amesema Kapuya.

Naye Mwamoto, aliahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha wananchi wote katika kushughulikia kero mbalimbali wilayani humo.

“Mimi natoka kwa mtemi Mkwawa sasa nimesikia kuwa hapa ndipo kuna makaburi ya Mirambo, hivyo sitaondoka mpaka mnilipe kwa niaba ya Mkwawa,” ametamba Mwamoto akitania.

error: Content is protected !!