January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kapteni Komba azidi kumliza Lowassa

Aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyayi Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Komba

Spread the love

WIKI moja tangu Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba (CCM) afariki dunia, Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa ameendelea kumlilia akimtaja kama mmoja wa makamanda wa kuongoza harakati za kumshawishi awanie urais. Anaandika Mwandishi wetu…(endelea).

Kabla ya kukumbwa na mauti, marehemu Komba alijipambanua kama mshirika mkubwa wa Lowassa, aliyeapa kumpigania ndani ya CCM kuhakikisha anagombea urais mwaka huu, akidai ndiye anayestahili kumrithi Rais Kikwete.

Katika kujipambanua huko kumpigania Lowassa agombee urais, maremu Komba alikaririwa akitamba kuwa tayari alikuwa ametunga nyimbo tatu kwa ajili ya kumnadi kada huyo ambaye hata hivyo hajatangaza rasmi kama ataingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Kutokana na ukaribu wa wawili hao, Lowassa kupitia kwa msaidizi wake, leo amesambaza taarifa ya tanzia yake kwa Komba akismea; “Ulipaza sauti bila woga kuelezea imani yako kwangu. Kapteni naumia sana umeondoka bila ya kukupa jibu la kukubaliana na ushawishi wako au la.

Tanzia ya Lowassa kwa Komba

>>>> Hivi ni kweli sitosikia tena sauti yako Captain Komba!, mbona umeondoka bila ya kuniaga ndugu yangu! Moyo wangu unabubujika machozi ya damu.
>>>>
>>>> Maneno yako kwa mmoja wa wasaidizi wangu siku tatu kabla ya umauti kukupata  kwamba “mwambie Edward akija aje kuniona mimi sijisikii vizuri” yanazunguka akilini mwangu.
>>>>
>>>> Captain Komba, Mimi na wewe tumepigana vita nyingi kwa maslahi ya chama na nchi yetu…na tulishinda vita hivyo. Lakini bado tulikuwa tunaendelea na mapambano ya kumnasua mtanzania katika umasikini.
>>>>
>>>> Komba ulikuwa muumini usiyeyumba wa “Safari ya Matumaini”. Ulikuwa mmoja wa makamanda wa kuongoza harakati za kunishawishi niwanie urais kupitia chama chetu. Ulipaza sauti bila woga kuelezea imani yako kwangu. Captain naumia sana umeondoka bila ya kukupa jibu la kukubaliana na ushawishi wako au la.
>>>>
>>>> Kwa hakika chama kimepata pigo. Ni nani asiyejua mchango wako katika ushindi wa chama chetu katika ngazi zote. Nyimbo zako ndiyo adhana au kengele ya kuwakusanya waumini (wana ccm na wananchi) katika mikutano ya chama. Komba ulikuwa nembo ya chama chetu.
>>>
>>> Komba umeondoka lakini umeacha alama katika ulimwengu wa siasa hususan katika chama chetu. Daima nitakukumbuka ndugu yangu, naamini kabisa yale mapambano utayaendeleza huko ulikoenda ambako sote tutakuja.

>>> Nakuahidi ndugu yangu kama tulivyokuwa pamoja katika matatizo na furaha zetu, mimi na chama chetu tutaendeleza pale ulipoachia kutatua matatizo ya familia. Namuomba mungu anipe nguvu na moyo wa kuyafanya hayo. Pumzika kwa amani rafiki yangu ipo siku isiyo na jina tutaonana.

error: Content is protected !!