December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kapteni John Komba afariki

Mbunge wa Mbinga Mgharibi, Kapteni John Komba enzi za uhai wake akiimba na bendi ya TOT

Spread the love

MBUNGE wa Mbinga Magharibi ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kapteni John Komba (60), amefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam majira ya saa kumi jioni.

Komba ambaye atakumbwa zaidi kwa umahiri wake wa kutunga na kuimba nyimbo mbalimbali za hamasa hususani za chama chake cha CCM, amekuwa mbunge kwa vipindi viwili tangu mwaka 2005.

Mwili wa John Komba baada ya kufariki katika hospitali ya TMJ
Mwili wa John Komba baada ya kufariki katika hospitali ya TMJ

Licha ya ugonjwa wake kutofahamika haraka, lakini kwa siku za hivi karibuni Komba amekuwa akihangaika kusaka matibabu katika hospitali za ndani na nje ya nchi.

Kapteni Komba Komba atakumbukwa kwa kauli yake ya kustaajabisha aliyoitoa katika Bunge Maalum la Katiba mwaka jana, dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, akimwita kuwa ni shida kwa CCM na hatari kwa muundo wa sasa wa serikali mbili.

Marehemu Komba alijiapiza kuwa ataingia msituni endapo mapendekezo ya wananchi ya serikali tatu yatapita. Licha ya kauli yake kuwashtua baadhi ya watu wakiwemo wajumbe wenzake, hakuna mamlaka yeyote ilimkemea.

error: Content is protected !!