KANSELA mpya wa Ujerumani, Olaf Scholz amelihutubia kwa mara ya kwanza bunge leo Jumatano, tarehe 15 Desemba 2021 na kuelezea miongozo ya miaka minne ya serikali yake iliyoingia madarakani wiki iliyopita. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).
Kansela Scholz ameliambia bunge hilo kwamba serikali yake itaipa nguvu zaidi Ujerumani na kujenga mustakabali wenye uhakika.
Aidha, Scholz amesema, kipaumbele chake ni kujenga Umoja wa Ulaya wenye mshikamano zaidi na kupambana na migawanyiko ambayo imekuwa ikiuathiri Umoja huo.
wa muungano wa kihafidhina CDU/CSU, Ralph Brinkhaus, amesema haoni dalili nyingi za maendeleo kwenye serikali ya muungano inayoongozwa na Scholz.
Chama cha siasa za wastani cha mrengo wa kushoto cha Social Democrats, kile cha kijani na kinachoegemea biashara cha FDP vilitia saini mkataba wa muungano mwanzoni mwa mwezi Disemba, takriban wiki 10 baada ya uchaguzi.
Scholz alichaguliwa na bunge kama Kansela wa tisa Ujerumani na kuchukua nafasi ya Angela Merkel baada ya miaka 16 madarakani.
Leave a comment