May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kanoute ‘Out’ dhidi ya Namungo

Spread the love

 

 KIUNGO mkabaji wa klabu ya Simba Raia wa Mali, Sadio Kanoute  hatokuwa sehemu ya kikosi cha klabu ya Simba kitakachoshuka dimbani kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa mzunguko wa pili utapigwa kesho tarehe 3 Mei, kwenye Uwanja wa Ilulu uliopo Lindi majira ya saa 10 kamili jioni.

Akizungumza na hali ya kikosi hiko mara baada ya kuwasili mkoani Lindi, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally alisema kuwa wamewasili mkoani humo nakikosi kamili isipokuwa mchezaji huyo aambaye alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Yanga.

“Tumefika salama Mtwara na tumekuja na wachezaji wote, isipokuwa Kanoute ambaye aliumia kwenye mchjezo uliopita dhidi ya Yanga, na amebaki Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.” Alisema Meneja huyo

Kwenye mchezo huo Kanoute alipata majeraha na kutolewa nje kwenye kipindi cha pili cha mchezo, kufuatia kuchezewa rafu mbaya na kiungo mkabaji wa klabu ya Yanga Khalid Aucho.

Kiungo huyo alijiunga na Simba kwenye dirisha kubwa la usajili mwezi Agosti, akitokea nchini Mali na kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza.

error: Content is protected !!