August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kanisa: Serikali iache kuigiza

Kanisa

Spread the love

MAADILI kwa watumishi wa umma yameporomoka kutokana na viongozi hao kutomjua Mungu, anaandika Dany Tibason.

Ni kauli ya Christopher Madole, Askofu wa Kanisa la Gospel Ministry Jimbo la Dodoma aliyoitoa leo alipokuwa akihubiri katika kanisa hilo lililopo viwanja vya Reli mjini Dodoma.

Alikuwa akiendesha ibada ya Siku ya Kumbukumbu ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo ambapo amesema, umefika wakati sasa wa wanasiasa na viongozi mbalimbali serikalini kuwa na hofu ya Mungu na sio kuigiza.

“… namshauri Rais Magufuli (Rais John Magufuli) aongeze wizara moja tu ya maadili ambayo waziri wake asitokane na chama chochote cha siasa.

“Maana tunaona kuna wakati mawaziri wanaonekana kutetea vyama vyao sasa hii wizara ya maadili itakuwa inasimamiwa na kiongozi wa kiroho,”amesema Askofu Madole.

Amesema kwamba, kutokana na kuporomoka kwa maadili, mawaziri na wabunge wamekosa aibu na hata kuwa na maneno ya kashfa ndani ya Bunge.

“Kumekuwepo na maneno ya kashfa hata ndani ya bunge, mfano; mbunge anasema sizungumzi na mbwa bali nazungumza na mwenye mbwa au kusikia mbunge anasema funga milango tupigane,” amesema.

Askofu Madole amesema kuwa, yote hayo ni dalili ya watu kukosa hekima na busara na zaidi ni kukosa hofu ya Mungu jambo ambalo ni hatari kwa viongozi na jamii kwa ujumla.

Kiongozi huyo wa imani amesema kwamba, wanasiasa sasa wamekuwa chanzo cha machafuko katika nchi zao kutokana na kuwa na tabia ya kutopenda kuachia madaraka sambamba na kukandaniza demokrasia.

Pia imeelezwa kwamba, wanasiasa wanakumbwa na tabia hiyo kutokana na kuwa na uchu wa madaraka jambo ambalo linatokana na kutokuwa na hofu ya Mungu.

Askofu Madele amesema yapo mataifa ambayo yanaingia katika machafuko kutokana na watawala wa nchi husika kukataa kutoka madarakani licha ya kumaliza muda wao.

Kiongozi huyo ametolea mfano wa rais wa Ghambia ambaye alishindwa katika uchaguzi mkuu wa urais na kukubali matokeo lakini muda mfupi alijitokeza na kupinga.

error: Content is protected !!