April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kanisa latoa somo kuongeza kinga ya COVID-19

Spread the love

KUSAMBAA kwa virusi vinavyosababisha homa kali ya mapafu (COVID-19), kumebadili mwenendo wa dunia. Anaripoti Dandons Kaijage, Dodoma…(endelea).

Prof. Pastor Majembe Chidachi, Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assembly of God (TAG), jijini Dodom amewaambia waumini hao, ni lazima kuwa waangalifu ili kujikinga na ugonjwa huo kwani ni tishio la dunia.

Ametoa taadhari wakati wa mahubiri yaliyofanyika kanisani hapo tarehe 22 Machi 2020, huku akieleza njia za kujikinga, kuzingatia taratibu za usafi na kula vyakula vyenye vitamin C.

Amesema, pamoja na kanisa kuendelea kufanya maombi kwa kuamini kuwa mponyaji pekee wa janga hilo ni Yesu Kristo, lakini pia kuna kila sababu ya kuzingatia sheia ambazo zinatolewa na wataalamu wa afya.

Kanisani hapo kukiwa kumeshehemi vitakatisha mikono ikiwa ni sehemu ya maelekezo ya wataalamu wa afya, mchungaji Majembe amesema, kila kaya iwe makini katika kujilinda na kulinda watoto ikiwa ni pamoja na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.

Kuhusu vyakula amesema, ugonjwa huo pia unaweza kukabiliwa na kinga ya kutosha ndani ya mwili, hivyo ni muhimu waumini na wananchi wote kwa ujumla wakazingatia ulaji wa vyakula vyenye vitamin C.

Ametaja vyakula hivyo kuwa ni pamoja na kula mbogamboga za majani hasa zenye rangi ya kijani. Kama vile mchicha, sukuma wiki, mchicha, matembele, spinachi, mnafu, kabeji majani ya kunde au maboga, ya maharage, majani ya muhogo (kisamvu) pamoja na pilipili hoho.

Vyakula vingine ambavyo utengeneza vitamin C ni nyanya mbichi pia hutupatia vitamini C.

Kwa upande wa matumda yenye kuwezesha vitamin C mwilini ni pamoja na matunda halisi hasa yenye tindikali kama vile machungwa, malimau, mapera, mabalungi, magogondi, matonga, zabibu iwapo yataliwa halisi (freshi), utengeneza kiasi kikubwa cha vitamaini C.

Vile vile Viazi vibichi, mihogo mibichi, magimbi na ndizi mbivu, zote kwa pamoja utengeneza vitamin C sambamba na ndizi za kupika.

error: Content is protected !!