June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kanisa laonya kuhusu siasa za Zanzibar

Spread the love

ASKOFU wa Kanisa la Mennonite Tanzania Dayosisi ya Kati, Amos Muhagachi, amewataka viongozi wa vyama vyote vya siasa nchi ya Zanzibar pamoja na asasi mbalimbali kutatua mgogoro uliopo kwa sasa. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Muhagachi alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kumalizika kwa ibada ya Jumapili iliyofanyika katika kanisa hilo jimbo la Iringa road mjini hapa.

Amesema ili kupata ufumbuzi wa kweli nchini Zanzibar ni jukumu la Wazanzibar wenyewe kukaa chini na wakaelewana na na siyo vinginevyo.

Askofu Muhagachi amesema kuna kila sababu ya vyama vyote vya siasa, asasi mbalimbali za kiraia na viongozi wa dini kwa kushirikiana na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wakakaa meza moja ili kutatua tatizo hilo.

“Hata kama inaonekana kuwa Zanzibar ni ndogo lakini ni nchi yenye Mamlaka kamili na ndiyo maana Zanzibar ina katiba yake hivyo ni jambo jema viongozi toka pande zote wakielewana ni rahisi zaidi kupatikana ufumbuzi.

“Pamoja na kuwepo kwa sababu nyingi za kufutwa uchaguzi lakini sababu hizo zikiwekwa wazi kuna uwezekano wa kurudia kuhesabu kura upya au kupiga kura kadri makubaliano yatakavyofanyika.

“Ni kweli kwa sasa uchumi umeshuka na unaweza kuendelea kushuka huko Zanzibar kama migogoro itaendelea maana hata watalii wanaweza kutofika, licha ya watalii hakuna mfanyabiashara anayejua nini kinaweza kutokea,” alieleza Askofu Muhagachi.

error: Content is protected !!