January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kanisa lamkingia kifua Askofu aliyefukuzwa

Spread the love

KANISA Anglikana Tanzania, limetoa ufafanuzi juu ya taarifa zilizodai kwamba wachungaji wa Kanisa Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza wamemfukuza Askofu Boniface Kwangu. Anaandika Dany Tibason, Dodoma …. (endelea).

Akitoa ufafanuzi wa jambo hilo Katibu mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania, Can. Capt. Johnson Chinyog’ole amesema si siyo kweli kuwa Askofu amefukuzwa.

Amesema kwa katiba na kanuni za kanisa Anglikani wachungaji hao hawana uwezo wa kumfukuza askofu huyo.

Amesema wamebaini kuwa kuna kikundi cha watu wachache ambao ni waasi ambao wanajaribu kutengeneza mgogoro ndani ya dayosisi hiyo.

“Kulingana na katiba ya Kanisa la Anglikana Tanzania Mamlaka pekee ya kumwomba askofu ajiuzulu au kustaafu kwa hiari ni askofu mkuu kwa kufuata katiba ya kanisa Anglikana Tanzania.

“Katiba ya kanisa imeweka sheria na kanuni za kushughulikia shutuma, malalamiko na mashitaka yanapotokea na kanisa kamwe hata siku moja halijapuuzwa kundi la watu wanaoleta hoja zao,” amesema katibu mkuu.

Katibu huyo amesema ni wajibu wa kila kasisi, mchungaji au askofu kuhakikisha anafanya kazi kwa kuzingatia kiapo ambacho ameapa.

Amesema kikundi cha wachungaji ambao wamejitangaza kuwa wana uwezo wa kumfukuza askofu kamwe watu hao hawana mamlaka na uwezo huo.

Katibu mkuu huyo akitoa ufafanuzi kwamba hakuna mchungaji yoyote anayeruhusiwa kutoa tamko lolote kuu pasipo kibali cha Askofu mkuu.

Amesema ni mila na desturi kanisa Anglilana Tanzania askofu huwa hafukuzwi hata kama kuna makosa yaliyothibitika, isipokuwa huombwa kustaafu au kujiuzulu.

error: Content is protected !!