January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kanisa Katoliki lamzuia Nkurunziza kuwania tena urais

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza akihutubia Mugikomero Wilayani Ngara

Spread the love

KANISA Katoliki nchini Burundi, lenye wafuasi zaidi ya robo tatu ya wananchi wote, limesema kuwa Rais anayemaliza muda wake, Pierre Nkurunziza hawezi kugombee muhula wa tatu katika uchaguzi ujao Juni mwaka huo.

Burundi iko kwenye mtanzuko wa ama Rais Nkurunziza, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2005, aruhusiwe kugombea kwa awamu nyingine ya tatu au la.

Hoja inayojengwa na wafuasi wake ni kwamba, kiongozi huyo wa zamani wa kundi la waasi mwaka 2005, alichaguliwa na Baraza la watunga sheria na sio wananchi wote kama ilivyokuwa uchaguzi wa 2010.

Chini ya Katiba ya Burundi, Rais anaruhusiwa kuhudumu kwa vipindi viwili pekee ikiwa atachaguliwa, lakini wafuasi wa Nkurunziza wanataka kipindi cha kwanza kisihesabiwe.

Nkurunziza mwenyewe bado hajatangaza kama atagombea wadhifa huo tena, japo wafuasi wake wanadhani anaweza kugombea.

“Tunawaomba wanasiasa walioyoko madarakani wasidhani au kuinukuu visivyo katiba. Vipengele vya kuhusu mihula ya rais viko wazi: Hakuna rais ataweza kuongoza nchi zaidi ya mihula miwili ya miaka mitano kila mmoja,” amesema Askofu mkuu wa kanisa hilo, Evariste Ngoyagoye, katika taarifa yake iliyosomwa Jumamosi.

“Mkataba wa makubaliano ya amani uliosainiwa na wadau wote wa kisiasa mwaka 2000 pia uko wazi; unasema kuwa kuanzia sasa, hakuna rais atahudumu zaidi ya mihula miwili,” ameongeza Ngoyagoye katika ujumbe huo ambao umetolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki nchini humo.

Tamko hilo kwa mara ya kwanza limefanya Kanisa Katoliki kuwa na upande rasmi katika mjadala unaoendelea juu ya uhalali wa Rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.

Kanisa hilo, limekuwa mshirika mkubwa katika mazungumzo ya kutafuta amani nchini Burundi.

Askofu Ngoyagoye amesema kuwa waumini wao, hivi karibuni, watafanya mafungo ya siku tisa nchi nzima kwa ajili ya kuombea amani ya nchi ili Rais Nkurunziza akabidhi madaraka kwa amani kwa mrithi wake.

error: Content is protected !!