KANISA Kuu la Kiaskofu la Jimbo Katoliki la Geita, limefungwa kuanzia jana Jumatatu hadi tarahe 18 Machi 2023, kwa ajili ya kusubiri utakaso wake baada ya kunajisiwa na mtu asiyejulikana. Anaripoti Mwandishi Wetu, Geita … (endelea).
Dikrii ya kufungwa kwa muda kanisa hilo imetolewa jana Jumatatu, tarehe 27 Februari 2023 na Askofu Jimbo Katoliki Geita, Flavian Kassala, ikiwa ni siku moja tangu mtu mmoja kuvamia na kufanya kufuru kwa kunajisi vifaa mbalimbslu vya ibada takatifu.
“Tukio hili ni uharufu mkubea sana ambao umeiathiri kwa kiasi kikubwa hadhi na muumini mkayoliki na jamii yetu kwa ujumla. Kutokana na matukio hayo kanisa hili limepoteza kwa kiasi kiku wa baraka yake kwa jamii,” imesema taarifa ya Askofu Kassala.
Taarifa hiyo imesema “waaminj wameumizwa sana kutokana na kashfa, kufuru na unajisi uliofanyika kwa imani yetu na hivyo naagiza kanisa hili halistahili kwa maadhimisho ya sakramenti ya ekaristi wala kwa ibada yoyote.”
Taarifa ya Askofu Kassala imesema kuwa, kanisa hilo litafunguliwa tarehe 18 Machi 2023, kwa adhimisho la ibada ya misa takatifu, itakayohusisha maadhimisho ya toba, malipizi na baraka.
Leave a comment