March 2, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kangi Lugola atengua uamuzi wake mwenyewe

Spread the love

SERIKALI imefuta utaratibu wa utoaji vibali kwa wananchi wanaolima jirani na kambi za wakimbizi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katazo hilo limetolewa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Wilaya ya Kankonko mkoani Kigoma baada ya kupokea malalamiko kutoka wananchi hao, kwamba utaratibu huo kuchelewesha shughuli zao.

Kufuatia malalamiko hayo, Waziri Lugola aliwataka wananchi wanaolima jirani na kambi za wakimbizi kuendelea na shughuli za kilimo pasipo kuomba kibali kama ilivyokuwa awali.

“Naagizia huu utaratibu ufutwe na wananchi wawe huru kwenda kulima katika maeneo ambayo yapo jirani na hiyo kambi pamoja na kambi zinginezo, na pia wasisumbuliwe na mtu yeyote, ” alisema Lugola.

error: Content is protected !!