July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kangi ataka wabunge kuwazomea mawaziri

Kangi Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Spread the love

MBUNGE wa Mwibala, Kangi Lugola (CCM), amewataka wabunge wenzake kuwazomea mawaziri ambao wamekimbia bajeti na badala yake kukimbilia kuwasaka wathamini kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kuomba kushika nafasi ya kuwa Urais. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kangi alitoa kauli hiyo bungeni alipokuwa akichangia katika hotuba ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2015/16 iliyowasilishwa bungeni hivi karibuni na Waziri wa Fedha Saada Mkuya.

Amesema  kuwa inasikitisha kuona mawaziri ambao wanahusika na masuala ya fedha wanakimbilia katika kutafuta wadhamini wakati wanashindwa kusimamia hata wizara moja ya elimu na majini.

Akichangia Kangi amesema  inasikitisha serikali kushindwa kuwalipa posho askari polisi wanapokuwa katika kazi zao za kila siku.

“Inasikitisha kuona serikali ambayo ina mawaziri ndani ya wizara husika lakini wanashindwa kutoa fedha za wizara moja na hao hao ndio wanazunguka nchi nzima kwa ajili ya kutafuta wadhamnini kwa kuomba ridhaa ya kuongoza taifa kwa nafasi ya urais”.amesema Lugola.

Anaongeza kuwa “Kama mtu anashindwa kuongoza wizara moja kwa kutoa fedha atawezaje kuziendesha wizara nyingi ndani ya serikali”

Akizungumzia kuhusu viwanda alisema ni aibu kwa serikali kuagiza kila kitu kutoka nchini china.

Alivitaja bidhaa hizo kuwa ni nyembe,pamba za kusafishia masikio,rula,vijiti vya kuchokonolea meno,jojo,kalamu za risasi,vichongeo vya karamu za risasi,chaki na vitu vingine vidogo vidogo.

Amesema kutokana na hali hiyo serikali imeshindwa kuimarisha viwanda na kutokana na hali hiyo ni wazi hakuna maendeleo ambayo yanaweza kujitokeza kwa wananchi.

“Serikali imeshindwa kusimamia viwanda kwatika uzalishaji wa mali licha ya kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuzalisha bidhaa mbalimbali kama kungekuwepo na viwanda vya kutosha” amesema

Nae mbunge wa Mbozi Magharibi David Silinde (Chadema), amesema  kuwa ufisadi mkubwa ndani ya serikali unatokana  na sheria ya manunuzi isiyokuwa na mashiko.

Amesema kutokana na kiburi  cha serikali ya CCM kujiona kuwa ni serikali ya kisultani imeshindwa kubadilisha sheria ya manunuzi ambayo inasababisha kuwepo kwa wizi mkubwa wa kutisha.

Akichangia katika hotuba ya Wizara ya fedha, Silinde amesema  serikali imekuwa ikibariki vitendo vya upotevu wa fedha kwa kushindwa kukusanya mapato kama inavyotakiwa.

“Nchi hii imekuwa ikiendeshwa na viongozi jeuri na wenye kiburi ambao wanadhani kuwa wataongoza nchi milele,kutokana na hali hiyo serikali imeshindwa kubadilisha sheria ya manunuzi ambako kwa kisi kikubwa ndiko unakofanyika wizi wa kutisha” amesema  Silinde.

error: Content is protected !!