February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kange Lugola atoa neno kupotea kwa mwandishi wa habari

Kange Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani. Picha Azory Gwanda

Spread the love
KANGE Lugola, Waziri wa Mambo ya Ndani, amesema wizara hiyo haihusiki na kupotea kwa mwandishi wa habari wa kampuni ya Mwananchi Communication Limited (Ltd), Azory Gwanda. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Lugola ametoa kauli hiyo, alipoulizwa msimamo wa wizara yake juu ya kupotea mwandishi huyo, Novemba mwaka jana.

Lugola amesema wizara yake haiingilii uhuru wa mtu kwani kitendo cha mtu kuondoka nyumbani kwake na kuelekea pasipojulikana kwani sheria za nchi hazimzuii mtu kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine kwani kufanya hivyo si kuvunja sheria.

Waziri Lugola amesema kama Gwanda alitoweka wakati akiwa nyumbani, wao hawahusiki bali wanahusika na mtu aliyetendewa uhalifu ikiwamo kutekwa, akisema katika tukio kama hilo vyombo vya dola humtafuta mtekaji.

“Hawa ambao wanatoweka kwao tu, wanakuwa na sababu nyingi. Kuna wengine maisha yakiwashinda anaamua kwenda kwingine,” amesema.

Lugola alieleza uzoefu wake alipotembelea migodi wakati  akiwa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). “Kwenye migodi nilikutana na watu ambao kwao walishaweka matanga kwa kujua wameshakufa. Kwao hawaonekani, lakini kumbe wametoweka,” alisema Lugola

Lugola ameeleza kuwa hicho ndicho anachoweza kusema kwa sasa kuhusu kutoweka kwa Gwanda.

Jeshi la Polisi, ambalo jukumu lake kubwa ni kulinda watu na mali zao, liko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

error: Content is protected !!