July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kane aomba kuondoka Tottenham

Harry Kane

Spread the love

 

HARRY Kane, mshambuliaji Tottenham Hotspur ameandika barua ya kutaka kuondoka kwenye klabu hiyo licha ya kubakia na mkataba wa miaka mitatu na kuhusishwa kujiunga na klabu za Manchester City, Chelsea na Manchester United. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kane mwenye umri wa miaka 27, anataka kuondoka kwenye klabu hiyo, ambayo alihudumu kwa kipindi cha miaka 12, licha ya kutowasilisha taarifa rasmi ya kwa maandishi.

Taarifa hizo zinakuja siku chache toka mchezaji huyo kunukuliwa kuwa “kwa sasa nahitaji timu ambayo nitashinda nayo mataji.”

Manchester City wanaongoza mbio za kumuwania mshambuliaji huyo, licha ya wamiliki wa klabu yake ya sasa kupambana kumbakisha kwenye viunga hivyo kwa kumuongezea mshahara.

Licha ya Manchester City kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kutafuta saini ya mshabuliaji huyo, mabosi wa Manchester United walijitanabaisha wazi ya kuwa wapo tayari kutoa kiasi cha Euro 90 milioni (sawa Sh. 250.8 bilioni) kumnasa mshambuliaji huyo.

Ndani ya Ligi Kuu England, Kane amecheza jumla ya michezo 33, nakupachika kambani mabao 22, huku akitoa pasi za mwisho (assist) 13 na kutengeneza nafasi 47.

Kane pia katika michezo hiyo amepiga jumla ya mashuti 51 yaliyolenga goli na kupiga pasi 870.

error: Content is protected !!