Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Kamwaga kuachana na Simba
MichezoTangulizi

Kamwaga kuachana na Simba

Ezekiel Kamwaga, Kaimu Afisa Habari wa Simba
Spread the love

 

EZEKIEL Kamwanga, amehitimisha safari ya mkataba wake wa miezi miwili ndani ya mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam. Anaripoti Damas Ndelema, TUDARCo … (endelea).

Kamwaga alianza kuitumikia Simba, tarehe 28 Julai 2021 kwa mkataba wa miezi miwili kama kaimu mkuu wa idara ya habari na mawasiliano.

Alipewa jukumu hilo, baada ya aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara kutangaza kuachana naye. Manara kwa sasa ni msemaji wa Yanga.

Katika kipindi cha miezi miwili aliyopewa Kamagwa aliyewahi kuwa kaimu katibu mkuu wa timu hiyo, alitakiwa kuboresha muundo wa utendaji wa idara hiyo ya habari.

Simba ilisema, mara baada ya kukamilika kwamaboresho ya idara ya habari na mawasiliano na idara nyingine, watatangaza fursa mbalimbali za ajira.

Kikao cha Bodi ya Simba

Kipindi hicho cha miezi miezi miwili, imemalizika leo Jumatatu, tarehe 27 Septemba 2021 na MwanaHALISI Online limedokezwa na kigogo mmoja wa Simba kwamba “Kamwaga hawezi kuongeza mkataba. Anakwenda masomoni London nchini Uingereza.”

Kigogo huyo amesema, jitihada za kumpata mrithi wa Kamwaga zinaendelea na haitachukua muda atatangazwa.

MwanaHALISI Online limemtafuta Kamwanga ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari amesema, suala hilo kwa sasa hawezi kulizungumzia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Vigogo wanaokwamisha mradi Liganga na Mchuchuma kitanzani

Spread the love  NAIBU Spika wa Bunge, Mussa Zungu, watu wanaokwamisha utekelezaji...

Habari MchanganyikoTangulizi

Hii hapa kauli ya Sheikh mpya mkoa wa Dar

Spread the loveSAA chache baada ya kuteuliwa kukaimu nafasi ya aliyekuwa Sheikh...

Habari MchanganyikoTangulizi

Breaking news! Mufti amng’oa Sheikh mkoa Dar

Spread the loveBARAZA la Ulamaa la Bakwata katika kikao kilichofanyika tarehe 1...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yatoa tamko bungeni sakatala la viboko shuleni

Spread the love  SERIKALI imewaagiza maafisa elimu wa mikoa na wilaya kuratibu...

error: Content is protected !!