Spread the love
KIUNGO wa wa Yanga, Thaban Kamusoko amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Desemba, 2015 baada ya kumshinda mchezaji mwenzake wa Yanga, Amissi Tambwe.
Kamusoko ameisaidia timu yake ya Yanga katika michezo iliyochezwa mwezi Desemba kwa kushiriki dakika zote katika michezo mitatu iliyochezwa mwezi wa Desemba.
Kwa kuchaguliwa kwake kuwa mchezaji bora wa wa mwezi Disemba, Kamusoko atakabidhiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni moja (1,000,000) kutoka kwa wadhamini wa ligi Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
More Stories
Manchester United kuivaa AC Milani, 16 bora Europa
Poulsen awabakisha Mgunda, Matola Taifa Stars
Kim awarudisha Yondani na Kessy Taifa Stars