January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kamukara afikishwa salama Muleba, kuzikwa kesho

Mwili wa aliyekuwa Mhariri wa MwanaHALISI Online, Edson Kamukara

Spread the love

MWILI wa aliyekuwa mhariri mwanzishi wa gazeti hili – MwanaHALISI Online – Edson Kamukara, umefikishwa salama kijijini kwao, Ihangiro, Muleba, mkoani Kagera. Anaripoti Desus Kahangwa, kutoka Muleba … (endelea). 

Mwili wa Kamukara ulipofika uliingizwa ndani ya nyumba ya mama yake mzazi, kabla ya baadaye kupelekwa kwenye sehemu ya kuhifadhia maiti iliyopo kijijini hapo.

Kifo cha Kamukara, kilitokea juzi Alhamisi, nyumbani kwake majira ya saa 12: 30 jioni, Mabibo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa familia ya marehemu, shughuli za mazishi zitaanza kesho (Jumatatu), majira ya saa 5 asubuhi ambako misa ya kumuombea marehemu Kamukara itafanyika nyumbani kwa mama yake mzazi.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika kati ya saa 9 jioni na saa 10.

error: Content is protected !!