Tuesday , 5 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Kampuni za upimaji zapigwa ‘stop,’ Goba yawa mfano
Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Kampuni za upimaji zapigwa ‘stop,’ Goba yawa mfano

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi 
Spread the love

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameagiza kampuni za upangaji na upimaji kutochukua kazi mpya kabla ya kumaliza kazi za awali. Anaripoti Hamis Mguta, Dar es Salaam … (endelea).

Lukuvi ametoa kauli hiyo leo tarehe 24 Februari 2020, wakati akizungumza na kampuni hizo jijini humo, kufuatia malalamiko ya wananchi katika maeneo mbalimbali, kuwa wamelipa pesa lakini kazi za urasimishaji hazijafanyika.

“Namuagiza Katibu Mkuu katika zoezi la urasimishaji, hakuna kuchukua kazi mpya mpaka hizi kazi tulizoanza nazo ziishe, nisisikie kampuni yoyote imechukua kazi mpya mahali popote hadi tarehe 30 mwezi wa nne,” amesema.

Aidha, ameagiza hamashauri zote nchini kutotoa kazi yoyote mpya kwa kampuni hizo, na kwamba Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Mary Makondo afanye tathmini ya namna gani wataingia kwenye utaratibu mpya baada ya kazi hizo kukamilika.

“Kuna watu kama kampuni ya Hosea, tangu 2017 hawamalizi kazi, makampuni yamekuwa na uchu wa kushika kazi lakini uwezo hawana, makampuni yamejiweka kwenye kazi nyingi ambazo uwezo wa kuzimaliza hawana,” amesema Lukuvi na kuongeza;

“Kazi zote ambazo hazijakamilika lazima zikamilike baada ya hapo tutakutana tuanze kazi mpya kwa makubaliano mapya, Katibu Mkuu na wewe ufanye tathmini ya kitaalam, tunaanza na utaratibu gani mpya. Nataka urasimishaji awamu inayokuja uwe na majibu,” amesema.

Renny Chuwa, Mwenyekiti Kampuni ya Upimaji ya Hosea ambayo imelalamikiwa zaidi na wananchi wa mitaa ya Goba – Kunguru, Msigani na Malimbika, kuwa imechukua pesa mida mrefu lakini haijakamilisha zoezi la urasimishaji amesema, kumekuwa na urasimu mkubwa katika upimaji na pia wananchi hawana uelewa wa kutosha juu ya zoezi hilo.

“Kampuni yetu ilipata shida mno, tunaweza kuumizwa leo Hosea na kesho akaumizwa mwengine hawa wananchi hawana makosa, kuna urasimu mkubwa kwenye baadhi ya viongozi ngazi ya halmashauri,” amesema.

Pamela Maro, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo amemuahidi Waziri Lukuvi kuwa, hadi kufikia tarehe 2 Machi 2020, maeneo yote yanayolalamikiwa yatakuwa yamerasimishwa na hati zitakuwa zimetolewa.

Hata hivyo, Waziri Lukuvi ameongeza wiki moja baada ya tarehe hiyo kwa ajili ya wizara kupata muda kupitisha michoro hiyo, ili ifikapo tarehe 9 Machi 2020 hati zote zilizokuwa zinagombaniwa ziwe zimekamilika.

“Walio wengi maeneo ya mijini wanaishi katika maeneo yasiyopimwa, asilimia 70 wanaishi katika makazi holela. Tumeajiri makampuni ya upimaji na upangaji ili yatusaidie kufanya kazi hii. Hatujasema wachukue kazi za serikali au serikali imeshindwa kazi,” amesema.

Aidha, Lukuvi amesema “yaliyozungumzwa na mashuhuda ni machache, na baadhi yake.

“Kwanza, tunapeleka mapendekezo bungeni kubadilisha sheria kutaka kila anayemiliki nyumba au ardhi mjini lazima alipe na kodi ya ardhi sio kodi ya nyumba pekeyake. Kuna watu wanaogopa kuchukua hati kwamba wakichukua, wataingia kwenye mlolongo wa kulipa kodi na kila anayepimiwa lazima achukue hati ili alipe kodi. Na hiyo sheria tutairekebisha mwaka huu.”

Amesema, pili; upo mgongano wa maslahi tunauona kwa baadhi ya wakandarasi, baadhi ya kazi za wapimaji binafsi zinacheleweshwa na watendaji wa serikali ambao wana kampuni binafsi.

“Baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri wamekuwa wanaajiri watendaji wa serikali kupima mitaani. Marufuku watendaji wa serikali kuchukua kazi ya taaluma yake binafsi nje ya serikali kwenye makamapuni binafsi,” amesema.

Na tatu Lukuvi amesema, baadhi ya watendaji wa halmashauri hawapitishi michoro hadi wapewe pesa. unakuta mchoro hauonekani kwasababu  haujatoa bahasha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake

Spread the love  MTANDAO wa Polisi wanawake wa Arusha kuelekea siku 12...

error: Content is protected !!