Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kampuni za simu zinazoruhusu meseji za matapeli, matangazo kikaangoni
Habari za Siasa

Kampuni za simu zinazoruhusu meseji za matapeli, matangazo kikaangoni

Nape Nnauye, Waziri wa Habari
Spread the love

 

WAZIRI wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuzichukuliwa hatua kampuni za mawasiliano ya simu zinazoruhusu meseji za matapeli na matangazo kufika kwa watumiaji kinyume cha sheria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Nape ametoa agizo hilo leo Jumanne, bungeni jijini Dodoma wakati anatoa ufafanuzi wa michango ya baadhi ya wabunge kuhusu sekta ya mawasiliano.

“Na watoa huduma za mawasiliano ambaye ataruhusu jambo hili tutachukua hatua bila shaka itakuwa suluhisho la jambo hili. Inatosha, meseji zimekuwa nyingi na mtandao wetu kwa hali ilivyo tukiendelea kuruhusu jambo hili nadhani tutakuwa hatuwatendei haki watumia huduma za mawasiliano,” amesema Nape.

Waziri huyo wa habari amesema, amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya ongezeko la meseji za matangazo mbalimbali na za matapeli ambazo wanatumiwa bila ridhaa yao, ambapo ameitaka TCRA kudhibiti changamoto hiyo.

Kwa upande wake Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, ameisisitiza wizara hiyo kuhakikisha meseji hizo zinadhibitiwa.

“Na kadri tunavyoenda yako mambo mengi kwa kweli inabidi kuyafanyia kazi, ikiwa pamoja na watoa huduma. matangazo kwenye simu zetu ni mengi sana na si yote ambayo wengine tunayahitaji hatujui hicho kibali wamejipa sababu tunatumia mitandao yao au wao wamefanya kukusanya taarifa mahali ambazo sasa zimeshalindwa kisheria,” amesema DK. Tulia na kuongeza:

“Matangazo kila aina yanatumwa, mkatazame kama kuna namna ya kujitoa wawe wanatutangazia kwamba mtu ambaye hataki matangazo ya namna hii piga namba hii namba yako itaondolewa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!