Monday , 26 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Kampuni ya ulinzi watuhumiwa kwa wizi UDOM
Habari Mchanganyiko

Kampuni ya ulinzi watuhumiwa kwa wizi UDOM

Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam
Spread the love

KAMPUNI binafsi ya ulinzi la Stemo Security imedaiwa kujiingiza katika vitendo vya kiharifu badala ya kufanya kazi zake za ulinzi wa mali za raia wanaowapatia tenda za ulinzi, anaandika Dany Tibason.

Hali ya kampuni hiyo kujihusisha katika tukio hilo la uharifu wa wizi unaofanywa na walinzi wa kampuni hiyo kwa kushirikiana na jamii kufanya wizi umebainishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mambosasa amesema katika msako mkali unaofanywa na jeshi la polisi mkoani Dodoma walibaini kuwepo kwa matukio ya wizi uliotokea katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Mambosasa amesema jeshi la polisi limewakamata watuhumiwa watano kwa makosa ya wizi wa pikipiki eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma, matukio yaliyoanza tangu 26 katika eneo hilo.

Amesema jumla ya pikipiki tano za wizi zilikamatwa katika msako unaoendelea na wezi wakubwa wa pikipiki hizo ni watu wenye dhamana ya ulinzi katika eneo la UDOM ambao ni kampuni ya ulinzi binafsi ya Stemo Security wakilishirikiana na watu wengine ambao mara baada ya kuiba wanazibadilisha namba na kazi na kuziuza maeneo ya vijiji vya mbande –Kongwa,Mtanana-Kongwa na Chipogolo-Mpwapwa.

Amezitaja pikipiki zilizokamatwa zikiwa na namba bandia na kadi za bandia ni, MC.523 BNK aina ya T-Better, pikipiki halisi iliyosajiliwa na TRA ni FEKON.

Nyingine kuwa ni MC 986aina ya T-Better, MC.824AQZ aina ya Boxer, MC 258 BQL aina ya Platnum, usajili wake halisi ni T-Better na MC 697 aina ya ZUNFAN inatumia tenki la FECON, usajili kamili wa TRA ni SUNLG.

Mambosasa amewataja watuhumiwa kuwa ni Daniel Isaya (30) mkazi wa Mbande, Lameck Sumiye (50) Kaimu Mkurugenzi wa Stemo Security mkazi wa Nghongh’onha, Ernest Sudayi (30) fundi ujenzi mkazi wa Iyumbu, Crement Kilei (43) mkulima na mkazi wa Mtanana wilayani Kongwa na Bariki Chitu (41) mkulina na Mkazi wa Chipogolo wilayani Mpwapwa.

Viongozi wa kampuni ya ulinzi ya Stemo kanda ya kati wakizungumzia tukio hilo wamesema waliokamatwa na polisi na kuhusishwa na wizi licha ya kuwa ni wafanyakazi wa kampuni hiyo lakini hawakufanya wizi wakiwa kazini.

Msimamizi wa kampuni hiyo kanda ya kati, Maliamungu Mgongolwa amesema mmoja wa watuhumiwa hao ni kijana ambaye alikuwa anafanya kazi katika kampuni hiyo na alikuwa akifanya vitendo vya wizi akiwa nje ya kazi kwa kushirikiana na watu wengine ambao siyo waaminifu.

Hata hivyo amesema ameviomba vyombo vya dola kumfungulia mashitaka kijana huyo kama mtu binafsi badala ya kumuhusisha na kampuni.

Akizungumzia aliyetajwa na polisi kwa kuhusika na wizi wa pikipiki kwa cheo cha kaimu mkurugenzi, Mgongolwa amesema jeshi la polisi limekosea kumpa cheo hicho kwani mtu huyo ni msimamizi wa walinzi wanaolinda katika UDOM.

Hata hivyo amesema ameviomba vyombo vya dola kumfungulia kesi Danieli Isaya kama mtuhumiwa binafsi badala ya kumuhusisha na kampuni ya ulinzi ya Stemo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RC Geita awafunda wahitimu wapya GGML

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito kwa...

Habari Mchanganyiko

Biteko asisitiza umuhimu wa EREA sekta ya nishati

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari Mchanganyiko

Tembo aongoza migongano binadamu, wanyamapori

Spread the loveIMEELEZWA kuwa asilimia 80 ya migongano baina ya binadamu na...

Habari Mchanganyiko

“Watanzania tembeleeni vivutio vya utalii”

Spread the loveSHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limewataka Watanzania kujitokeza kutembelea...

error: Content is protected !!