August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kampuni ya Mbowe yavamiwa

Spread the love

OFISI za gazeti la kila siku linalomilikiwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tanzania Daima zimevamiwa na mawakala wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), anaandika Faki Sosi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio na kuthibitishwa na Neville Meena, Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo linaloendeshwa chini ya Kampuni ya Free Media zinaeleza kuwa, mawakala hao Kampuni ya Action Mark, wamefika asubuhi na kuanza kutoa vifaa kwenye ofisi hizo.

“Madalali wa NHC wamefika ofisini kwetu asubuhi hii na kuanza kutoa vifaa vyetu ofisini…,” amesema Meena.

Hivi karibuni NHC imeeleza kumdai Mbowe jumla ya Sh. 1.3 Bilion kama kodi kutokana na kampuni yake ya Hotels Limited (MHL) kukodi jingo la shirika hilo.

Jengo hilo lipo katika makutano ya Mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi (Makunganya) jijini Dar es Salaam.

Jengo hilo ni maarufu kutokana na kuendesha shughuli mbalimbali za starehe na burudani kutokana na kuwepo kwa Club maarufu ya Billicanas.

Hatua hiyo inatokana na notisi iliyotolewa NHC Juni 24, mwaka huu, ikitishia kuvunja makubaliano ya mkataba wa ukodishaji wa jengo hilo. Taarifa zaidi zitakujia

error: Content is protected !!