May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kampuni ya Coastal yaandika historia Afrika kwa kubeba cheti cha usalama kutoka IATA

Spread the love

 

USALAMA ni moja ya nguzo muhimu katika masuala ya usafiri wa anga. Hiki ndio kigezo ambacho kimezishinda kampuni nyingi za usafiri wa anga Barani Afrika kushindwa kushindana na makampuni makubwa. Hata hivyo sasa hali ni tofauti kwa upande wa kampuni ya Coastal Travels Limited. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hivi karibuni kampuni hiyo ya Coastal Travels Limited ilifanikiwa kupata cheti cha tathmini ya Kiwango cha Usalama kutoka Jumuiya ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (ISSA). Coastal inakuwa kampuni ya kwanza Barani Afrika kupata kupata cheti hicho ambacho kimesanifiwa kwa jili ya usafiri wa abiria kibishara, ubebaji wa mizigo.

Mpango wa ISSA ni kiwango cha usalama kwa mashirika ya anga duniani yanayoendeshwa kibiashara. Programu ya Tathmini ya Usalama wa Kiwango cha IATA (ISSA) ni mfumo wa tathmini unaotambuliwa na kukubalika kimataifa wa kutathmini uendeshaji  na usimamizi wa mifumo ya ndege.

Mafanikio haya yanalandana na malengo ya Kampuni ya Geita Gold Mining Limited pamoja na Coastal Travels Limited kwa kuzingatia masuala ya usalama. Kwa kuzingatia soko la kisasa kuhusu usafiri wa anga, hasa athari za kimazingira zilizowakumba abiria, ni muhimu kwa waendeshaji wa mashirika ya ndege kuboresha na kuzingatia  viwango vyao vya usalama.

Haya ndiyo mafanikio ambayo Coastal Travels Limited imeyapata kwa kutunukiwa cheti cha udhibitisho kutoka IATA. Coastal Travels Limited ambao ni waanzilishi wa usafiri binafsi wa anga nchini Tanzania. Coastal wamepokea hati hii ya ISSA kutoka IATA ili kudhibitisha kuwa ni kwa namna gani wanafuata viwango vya usalama vinavyotambulika ulimwenguni na vigezo vinavyopendekezwa kwa ujumla.

Coastal kwa sasa ndiye mwendeshaji pekee barani Afrika mwenye usajili wa ISSA. Ili kupata cheti hicho, mifumo ifuatayo ya usimamizi na udhibiti wa Coastal Travels Ltd. ulitathminiwa kwa kina na IATA ili kupata kiwango cha vigezo vyote vya ISSA  wanavyostahili kupatiwa.

Viwango na vigezo vilivyokuwa vimependekezwa ni ; Usimamizi wa Shirika (ORG),  Uendeshaji wa Ndege (FLT),  Matengenezo na Uhandisi (MNT),  Udhibiti wa shughli za uendeshaji na Utumaji mizigo (DSP), Utunzaji wa eneo la kiwanja cha ndege kurukia (GRH), Mizigo (CGO) na Usalama (SEC)

Kufuatia tathmini na taratibu anuwai za kudhibiti ubora, Jumuiya ya Usafiri wa Anga wa Kimataifa (IATA) ilihitimisha kazi hiyo Juni 18, 2021 na kuidhinisha kwamba Coastal Travels Limited inastahili kujumuishwa katika orodha ya mashirika salama ya ndege yaliyoidhinishwa kupewa ISSA duniani.

Faida ya kupata udhibitisho huo wa kipekee ulioletwa Coastal ambao pia ni wa Geita Gold Mining Limited na washirika wa kibiashara kwa wateja wa kampuni hiyo ya GGML ni pamoja na Kupunguza ukaguzi wa ziada, faida za kimasoko na kibiashara kama vile ushirikiano wa pamoja kwa makampuni ya ndege, kupunguza malipo ya bima,  ni hatua ya awali ya IOSA (Ukaguzi wa Usalama wa Uendeshaji kutoka IATA), Upimaji wa malengo yanayotarajiwa kufuatwa na Coastal pamoja na utekelezaji wa Mfumo wa Usimamizi wa Usalama (SMS).

Hakika haya ni mafanikio ambayo tumepata! Wafanyakazi wote wa Coastal wanathibitisha kuendelea kutoa huduma bora , za kuaminika, na salama kwa wageni wote.

“Tumejikita katika kuhakikisha kuwa usalama uko juu kabisa kipaumbele cha kwanza kwenye kampuni. Baada ya miaka miwili ya mafunzo na tathmini madhubuti ya marubani wetu na kuanzishwa kwa kwa chumba maalumu cha ndege cha MCC,  sasa tunazidi kuboresha huduma zetu zaidi,”alisema Kapteni Maynard Mkumbwa, Mkurugenzi Mtendaji wa Coastal

Aliongeza kuwa timu ya Coastal hupitia tathmini ya mara kwa mara. Huangalia kila siku shughuli zao za kila siku na kuhakikisha wanafuata taratibu za Uendeshaji (SOPs). Ni safari ya kudumu  na ngumu kufikia mafanikio haya ambayo kampuni imefikia lakini lengoi letu ni kuleta huduma za uhakika kwa abiria wetu.

“Hali hii ya kutokuwa na wasiwasi ndio inayotufanya tuwe macho na wasikivu. Mafunzo na tathmini inayoendelea ya marubani wetu yameleta mabadiliko makubwa kwani tumeanzisha idara ya viwango inayohusika na kuhakikisha kuwa marubani wetu wote na ndege zetu zote zinakidhi kiwango cha Coastal.Tunazingatia maoni kutoka vyanzo mbalibali ikiwamo hata ripoti zetu za ndani za ukaguzi, maoni kutoka kwa wateja na waendeshaji wengine ili kuifanya kampuni hii kuwa ya kisasa “- Kapteni Mkumbwa anasema.

Anasema safari hii ya kukuza viwango vya juu vya usalama na utendaji ni mchakato endelevu ambao unahitaji umakini na uamuzi mgumu.

Coastal Travels Limited ni mojawapo ya kampuni iliyopata bahati ya kuwa na Mkurugenzi Mtendaji mpya, Kapteni Maynard Mkumbwa ambaye amefanya kazi kwa Coastal Travels Limited kwa zaidi ya miaka 20 na ana zaidi ya miaka 30 ya uzoefu wa kitaalam katika tasnia ya anga.

error: Content is protected !!