Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kampeni ya ‘Vuna zaidi na NBC Shambani’ yawavutia wakulima wa Korosho Lindi na Mtwara
Habari Mchanganyiko

Kampeni ya ‘Vuna zaidi na NBC Shambani’ yawavutia wakulima wa Korosho Lindi na Mtwara

Mratibu wa uwekezaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Gaudence Nyamwihura (katikati) akijaribu ubora wa moja ya matrekta yatakayotolewa kwa washindi wa kampeni ya ‘Vuna zaidi na NBC Shambani'
Spread the love

 

CHANGAMOTO ya huduma za kifedha iliyokuwa ikiwakabili wakulima wa korosho mikoa ya Mtwara na Lindi ikiwemo kutopata mikopo kwa wakati na makato ya fedha zao wanapofanya miamala ya kibenki, imetajiwa kuwa miongoni mwa sababu kubwa zilizopelekea wakulima hao kuvutiwa zaidi na Kampeni ya ‘Vuna zaidi na NBC Shambani’ inayoendeshwa na benki ya NBC mahususi kwa mikoa hiyo.  Anaripoti Patricia Kighono, TUDARCo … (endelea). 

Wakizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo mkoani Lindi jana tarehe 22 Septemba 2021, na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa zao hilo wakiwemo viongozi wa kiserikali, viongozi vyama vya msingi (AMCOS) na vyama vikuu vya ushirika, wakulima hao walisema ujio wa kampeni hiyo umewahamasisha zaidi kujiunga na huduma ya NBC Shambani ili waweze kujikwamua kutoka kwenye changamoto hizo zilizotajwa kukwamisha jitihada zao za kujikwamua na umaskini kupitia kilimo cha zao hilo.

“Pamoja na uwepo wa zawadi mbalimbali kwenye kampeni hii ikiwemo baiskeli, pikipiki, pampu za kupulizia dawa, maguta  pamoja na matrekta zaidi pia tumevutiwa sana akaunti husika kwa kuwa inajibu changamoto kadhaa zinazotukabili kwenye huduma za kifedha ikiwemo ucheleweshwaji wa mikopo na makato yaliyokithiri,’’ alisema Swalehe Juma, Mwenyekiti wa Nachunyu AMCOS iliyopo mkoani Lindi.

Mmoja wa wadau wa zao la korosho kutoka mkoani Lindi akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Vuna zaidi na NBC Shambani’ mahususi kwa wakulima wa korosho mikoa ya Lindi na Mtwara.

Walisema changamoto ya ucheleweshwaji wa mikopo imekua ikisababisha wengi wao kupata fedha wakati usio sahihi kulingana na mahitaji yao ya kilimo na hivyo kujikuta wakitumia mikopo hiyo kwa shughuli zisizoendana na kilimo.

“Tunashukuru kuona kwamba NBC wameamua kubuni huduma mahususi kwa ajili yetu… tukiwa kama viongozi wa vyama vya msingi tumeipokea vema huduma hii na tumejipanga kuhakikisha kwamba inawafikia wanachama wetu wote kwenye maeneo yetu,’’ aliongeza.

Akizungumza zaidi kuhusu kampeni hiyo, Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Raymond Urassa alisema licha ya uwepo wa huduma ya NBC Shambani kwa zaidi ya mwaka sasa benki hiyo imebuni kampeni hiyo ili kuhakikisha kila mkulima wa korosho anafikiwa na huduma hiyo ili kwa pamoja waweze kufikia adhma ya kuleta mapinduzi ya kilimo kupitia zao hilo.

“Vuna zaidi na NBC Shambani’ ni kampeni inayolenga kuhamasisha mapinduzi ya kilimo cha korosho katika mikoa ya Lindi na Mtwara na ndio sababu hata zawadi zinazotolewa kupitia kampeni hii ikiwemo pikipiki, pampu za kupulizia dawa na matrekta  zinalenga kumsaidia mkulima aweze kustawisha kilimo chake,’’ alifafanua.

Akizungumza wakati akifungua kampeni hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mratibu wa uwekezaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Gaudence Nyamwihura pamoja na kuwasisitiza wakulima hao na AMCOS kuchangamkia kampeni hiyo, pia aliwasisitiza kubainisha vipaumbele vyao pindi wanapoamua kukopa kwenye taasisi za kifedha ili matumizi ya mikopo hiyo iwe na tija zaidi kwao.

Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wakulima kutoka Benki ya NBC, Raymond Urassa akitoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa zao la korosho

Uzinduzi wa kampeni hiyo ulienda sambamba na uzinduzi wa huduma ya Bima ya afya kwa wakulima wa zao hilo inayotolewa na benki hiyo kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) pamoja utoaji wa msaada wa pikipiki na baiskeli zilizotolewa na benki hiyo kwa AMCOS mbalimbali za mkoa huo kwa ajili ya kurahisisha shughuli za kiutendaji kwa AMCOS hizo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!