Saturday , 3 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Kampeni ya Samia Legal Aid yazinduliwa Manyara, kesi 45 zapokelewa
Habari Mchanganyiko

Kampeni ya Samia Legal Aid yazinduliwa Manyara, kesi 45 zapokelewa

Spread the love

 

KAMPENI ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, imezinduliwa mkoani Manyara, ambapo mamia ya wananchi wamepatiwa huduma hiyo na wasaidizi wa kisheria kutoka Shirika la Legal Services Facility (LSF). Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara … (endelea).

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Programu na Uendeshaji kutoka LSF, Amani Manyelezi, amesema kwa mwaka huu kampeni hiyo imelenga kuwafikia watu 7,000,000.

Manyelezi amesema katika uzinduzi huo, kesi 45 zimepokelewa na kufanyiwa kazi.

“Kampeni hii imeenda sambamba na kazi tunazozifanya kwa takribani miaka 11 za kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wote kupitia watoa huduma zaidi ya 4,000 waliopewa mafunzo ya kisheria nchi nzima Tanzania bara na Zanzibar,” amesema na kuongeza:

“Kwa mwaka tunawafikia watu million 7 kupitia elimu ya kisheria. Vilevile tunapokea migogoro takribani 70,000 ambapo asilimia 60 inatatuliwa na wasaidizi wa kisheria na hivyo kupunguza msongamano mahakamani. Kampeni hii ina tija kubwa kwetu kwani tumepanga kufikia maeneo, ambayo ni ngumu kufikiwa na huduma hizi, hivyo tumejipanga kushirikiana na Serikali kimalilifu katika kutekeleza na kufikia malengo yetu.”

Baada ya kampeni hiyo kuzinduliwa mkoani Manyara, itaendelea kufanyika kwa muda wa siku 10 mfululizo, katika wilaya zote za mkoa huo.

Kampeni hiyo imeanzishwa nchi nzima kwa ajili ya kulinda na kukuza upatikanaji haki kwa wote kupitia huduma ya Msaada wa Kisheria na itafanyika katika kipindi cha miaka mitatu.

Mbali na uimarishaji haki, kampeni hiyo imelenga kutatua migogoro ya kisheria kwa wananchi na kuweka mazingira wezeahi ya upatikanaji wa huduma ya kisheria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Magunia 731 ya bangi yakamatwa, mamia ya hekari yateketezwa Arumeru

Spread the love  MAMIA ya magunia ya madawa ya kulevya aina ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

error: Content is protected !!