January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kampeni ya Kubenea J’pili

Spread the love

MGOMBEA Ubunge Jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Saed Kubenea atafungua rasmi pazia la kampeni zake katika kuwania nafasi hiyo Jumapili ya tarehe 13 Septemba mwaka huu. Anaandika Pendo Omary … (endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online Katibu wa Kubenea, Elizabeth Mbombo amesema kampeni hizo zitazinduliwa saa 8 mchana hadi saa 12 jioni katika viwanja vya Mpakani karibu na Mahakama ya Ndizi, Mabibo ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye.

Sumaye alijiunga na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) mwezi mmoja uliopita baada ya kile alichokiita “chama kumekuwa kikikiuka misingi na wajibu wake kwa Watanzania.”

Mbombo  anasema, “mpaka sasa kwa kiasi kikubwa maandalizi yanaendelea vizuri. Mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye. Mkutano utarushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha ITV. Pia watakuwepo wasaamii mbalimbali wakiwemo Msaga sumu na G Five.”

Elizabeth anatoa wito kwa wakazi wa ubungo na Jiji la Dar es Slaam kuhudhuria mkutano huo na kusikiliza vipaumbele vya mgombea uhuyo na chama chake ili kufanya maamuzi sahihi wakati wa kupiga kura 25 Oktoba mwaka huu.

error: Content is protected !!