January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kampeni kusomesha watoto 112

Wanafunzi wa shule ya msingi wakiwa wamekaa chini baada ya kukosa madawati

Spread the love

Shirika lisilo la kiserikali la The Foundation for Tommorow limezindua kampeni  ya kuchangia  SHAMIRI ya kusaidia elimu ya watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu. Anaandika Ferdinand Shayo, Arusha … (endelea).

Aidha, lengo ni kuchangisha  kiasi cha shilingi milioni 50 zitakazowawezesha kupata elimu bora na kuondokana na mazingira yanayowakabili Meneja Mahusiano wa shirika hilo Anton Asukile amesema wakati akizindua  kampeni  maalumu ya SHAMIRI  inalenga  kusaidia ustawi wa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

Kampeni hii itawezesha kuinua uchumi wa kaya 40  za watoto  wanaoishi katika mazingira hatarishi  kupitia mradi wa WEZESHA KAYA pia itasaidia upatikanaji wa vifaa muhimu vya kujifunzia kwa watoto wapatao 112.

Amesema  Asukile Asukile ameiomba jamii ya Watanzania kushiriki  katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili jamii ili kuwakomboa watoto wanoishi katika mazingira hatarishi kwa kuchangia kampeni ya SHAMIRI.

Amesema kuwa Watanzania wataweza kuchangia fedha hizo kwa njia ya simu katika  kampeni hiyo imeanza rasmi mwenzi Julai na itahitimishwa septemba 25 mwaka huu.

Meneja Programu wa masuala ya kijamii na afya Hedwiga amesema kuwa baada ya kutoa misaada kwenye familia duni wameona ni vyema wakazipatia mafunzo ya ujasiriamali na mikopo ili waweze kujikwamua na kusomesha watoto wao pasipo kutegemea misaada.

Hedwiga ameitaka jamii ya watanzania kuamka na kusaidia watoto yatima na wanaotoka kwenye familia masikini badala ya kusubiri mashirika kutoka nje yaje kutoa misaada.

error: Content is protected !!