May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Kampeni Buhigwe: Majaliwa amwaga sera, ahadi

Kassim Majaliwa, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM alipokuwa akizungumza na wakazi wa jimbo la Muhambwe

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imetenga zaidi ya Sh.1 bilioni kwa ajili ya kuboresha hospitali ya wilaya Kibondo, mkoani Kigoma, ili kuhakikisha wakazi wa wilaya hiyo, wanapata huduma bora za afya. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea)

Kauli hiyo imetolewa na jana Jumanne, tarehe 4 Mei 2021, na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa, alipokuwa akizungumza na wakazi wa jimbo la Muhambwe, wilayani humo, kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Kibondo mjini.

Majaliwa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa Tanzania, alisema Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni humo, hivyo wamchague Dk. Frorence Samizi, kwa kuwa ndiye atakayeweza kusimamia miradi hiyo.

Alisema, anawaomba wakazi wa jimbo la Muhambwe wamchague Dk. Frorence, kuwa mbunge wa jimbo hilo kwani ndiye atakayewaletea maendeleo.

“Mchagueni mgombea kutoka CCM, kwa sababu ndiyo chama kinachowahudumia wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote, inawahudumia watu wake bila ya kujali uwezo wa kifedha, wala ukabila, tumchague Dk. Frorence atuletee maendeleo,” alisema Majaliwa.

“Uchaguzi hauhitaji ushabiki wala mbwembwe bali umakini mkubwa ili kumpata kiongozi atakayekuwa mstari wa mbele kuwatumikia na kuwasemea mahali popote naye si mwingine ni Dk. Frorence,” alisema

Majaliwa alisema, wakimchagua watarahisisha shughuli za maendeleo katika jimbo hilo zikiwemo za ujenzi wa miundombinu mbalimbali kama afya na barabara.

“Wana-Muhambwe wote twende na Dk. Frorence kwa maendeleo ya jimbo letu,” alisema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kasulu vijijini, Augustino Vuma amewaomba wakazi wa jimbo hilo la Muhambwe wamchague Dk. Frorence kwa sababu ni kiongozi mnyenyekevu, msikivu na ndiye atakayeweza kushirikiana nao katika kutatua changamoto zinazowakabili.

Naye, Dk. Frorence ametumiwa fulsa hiyo kuwaomba wakazi wa jimbo hilo kumpigia kura nyingi za ndio ili awe mwakilishi wao atakayeshirikiana nao katika kuhakikisha jimbo hilo linapata maendeleo.

Uchaguzi wa Jimbo hilo, utafanyika tarehe 16 Mei 2021, baada ya aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo, Atashasta Nditiye wa CCM, kufariki dunia katika ajali ya gari, jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

error: Content is protected !!