Spread the love

 

KAMISHNA wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) William Mwakilema leo Jumatano tarehe 23 Machi 2022 amewavisha vyeo Makamishna Wasaidizi wa Uhifadhi waliopandishwa vyeo hivi karibuni katika tukio lililofanyika Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara. Anaripoti Mwandishi Wetu, Manyara … (endelea).

Waliovalishwa vyeo ni Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Fidelis Kapalata na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Moses Nonga ambao kabla ya hapo walikuwa Maafisa Wakuu wa Uhifadhi.

Kamishna wa Uhifadhi William Mwakilema amewataka Makamishna wapya kufanya kazi zao kwa kuzingatia viapo vyao, weledi, bidii na maarifa ili kulifanya shirika lisonge mbele katika majukumu yake ya uhifadhi.

“Ni vema tufanye kazi kama timu moja kwa ushirikiano, tuwe mfano kwa tunaowaongoza pamoja na kuwajengea uwezo wa kushika nafasi za uongozi hapo baadaye,” amesema Mwakilema.

Kamishna Msaidizi Fidelis Kapalata kwa niaba ya mwenzake aliahidi ushirikiano kwa viongozi wenzake wa shirika ili kuweza kufikia malengo tarajiwa ya shirika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *