Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Kamishna Makarani wa ZAECA ajiuzulu
Habari Mchanganyiko

Kamishna Makarani wa ZAECA ajiuzulu

Spread the love

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA), Ahmed Khamis Makarani amejiuzulu. Anaripoti Jabir Idrissa, Zanzibar … (endelea).

Makarani ambaye ni ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi Tanzania mwenye cheo cha Kamishna Msaidizi – Assistant Commissioner of Police (ACP), ameandika barua ya uamuzi wake huo na kumkabidhi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ambaye ameridhia uamuzi huo.

Taarifa ya kujiuzulu kwa ACP Makarani imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Charles Hillary kupitia taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari jioni leo Ijumaa.

“Rais wa Zanzibar amekubali barua ya kujiuzulu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar,” imesema taarifa hiyo ikieleza kuwa ni hatua inayofuatia kauli ya Rais Dk. Mwinyi kutaka uongozi ujitathmini.

Rais Dk. Mwinyi alitoa kauli hiyo wakati akihutubia hadhara ya viongozi mbalimbali baada ya kupokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Zanzibar (CAG) ya mwaka 2020/2021.

Ripoti hiyo imeeleza kasoro nyingi za matumizi ya fedha za serikali zinazosababisha ubadhirifu wa mamilioni ya fedha.

Rais Dk. Mwinyi akionesha kukerwa na ufisadi serikalini alisema anashangaa kukuta matatizo hayo yanajirudia na hakuna hata mtuhumiwa mmoja aliyefikishwa kwenye vyombo vya kisheria.

Alisema anashangaa kwamba hakuna kesi hata moja iliyopelekwa mahkamani wakati ofisi yake imekabidhi kwa Zaeca ripoti yenye maelezo thabiti ya namna ufisadi ulivofanyika na wahusika kutajwa na baadhi yao kukiri na kurudisha fedha.

“Hatuwezi kuendelea hivi wizi kila mahali na hakuna kesi iliyopelekwa mahkamani… kwa namna hii inabidi ZAECA mjitathimini. Hatuwatendei haki wananchi,” alisema baada ya kusikiliza maelezo ya saa nne mfululizo ya CAG Dk. Othman Abbas Ali akieleza namna mabilioni ya fedha zilivyopotea huku maofisa masuuli wakikosa maelezo ya zilivyotumika.

Written by
Jabir Idrissa

+255 774 226248

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!