Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kamisha mpya TRA apewa majukumu mazito
Habari za Siasa

Kamisha mpya TRA apewa majukumu mazito

Dk. Edwin Mhede, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Spread the love

DAKTARI Edwin Mhede, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ameapishwa leo huku akipewa majukumu mawili mazito. Anaripoti Bupe Mwakiteleko … (endelea).

Kwanza ametakiwa kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato; pili kurudisha uhusiano mwema kati ya TRA, wafanyabiashara na walipa kodi wote nchini.

Majukumu hayo amepewa na Dk. Phillip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango leo tarehe 10 Juni 2019 katika hafla ya kuapishwa kwake iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam. Pia ameapishwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Dk. Mpango amemtaka Mhede kushirikiana vyema na watendaji atakaowakuta katika utekelezaji wa majukumu hayo.

Dk. Mpango amesema, wakati akikaimu nafasi ya Ukamishna Mkuu wa TRA, aliongeza kasi ya ukusanyaji mapato kutoka kiasi cha Sh. 850 Bilioni hadi kufikia Trilioni 1.3 na kumtaka Dk. Mhede kuhakikisha kwamba, kasi hiyo inarejea maradufu.

“Dk. Mhede karibu TRA, kuna changamoto lakini nitangulie kusema kwamba mtangulize Mungu. Mara ya kwanza ambako tuliongeza ukusanyaji mapato takribani Sh. bilioni  850 ni mimi wakati nakaimu.

“Tulifikia Trilioni 1.3,  toka wakati ule wastani ule unazunguka hapo hapo kila mwezi, lakini mahitaji yetu ni makubwa. Una kazi kubwa ya kuhakikisha tunaondoka kwenye huo mnato,” amesema Dk. Mpango.

“Changamoto ya pili, sura ya TRA ina matope kwa maana ya mahusiano yenye mushkeri ya wafanyabiashara na walipa kodi, unayokazi kubwa ya kushirikiana na wenzako utakao wakuta kuisafisha sura ya TRA iwe ni mamlaka ambayo wafanyabaishara na walipa kodi wote wanatambua kwamba ni chombo chao,” amesema Dk. Mpango.

Hata hivyo, Mhode akizungumza baada ya kuapata nafasi amesema kuwa, majukumu aliyokabidhiwa na serikali ni makubwa na kwamba, anatambua unyeti wa suala hilo.

“Majukumu uliyonipa si madogo, natambua unyeti wake kwa msingi huo nisingpenda kuongea mambo mengi zaidi ya kuhakikishia kwa umri wangu, sipaswi kukuangusha. Nikuhakikishie siogopi kitu chochote.

“Siwezi kuogopa ilhali najua kazi hii inaenda kuamua maisha ya watanzania milioni 55. Naelewa nilipewa jukumu hili, namtegemea Mungu…nakuhakikishia sio kwamba nitasimamia misingi hiyo,” amesema Mhode.

Kwa upande wa Bashungwa, Dk. Mpango amesema, anamuombea heri katika utekelezaji wa majukumu yake, huku akimhakikishia kwamba yuko tayari kumpa msaada wa hali na mali muda wowote atakaohitaji.

“Bashungwa, wizara ya viwanda unayokwenda kusimamaia huko ndiko ninakopata kodi, sababu na mimi sina uwaziri wa fedha bila kukusanya mapato na kuombea kheri, na nitakua tayari kabisa kutoa ushauri wangu muda wowote utakaouhitaji,” amesema Dk. Mpango.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Mwakyembe : Zanzibar waliongoza kutaka Serikali 2 za muungano

Spread the love  MWANASIASA mkongwe nchini, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema mjadala wa...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia ataja mikakati ya kufikia trilioni 2 biashara Uturuki, Tz

Spread the loveWakati Tanzania na Uturuki zikidhamiria kuongeza kiwango cha biashara hadi...

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

error: Content is protected !!