Saturday , 22 June 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kambi ya Upinzani wajipanga kumng’oa Spika Ndugai
Habari za SiasaTangulizi

Kambi ya Upinzani wajipanga kumng’oa Spika Ndugai

Job Ndugai
Spread the love

KAMBI rasmi ya upinzani Bungeni imepanga msimamo wa kumng’oa Spika wa Bunge, Job Ndugai iwapo hatabadilisha  msimamo wake wa kutangaza kuwa Bunge limesitisha kufanya kazi na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kambi hiyo ilisema kuwa shughuli za Bunge zinaendeshwa kwa misingi ya sheria na Kanuni ndani ya bunge na nje ya Bunge na kamati mojawapo iliyopewa mamlaka katika masuala yanayohusiana na utendaji wa Bunge kama bunge lenyewe halijakaa kikao ni kamati ya uongozi ya Bunge ambayo ndani yake kuna kiongozi wa Kambi ya Upinzani au mwakilishi wa Kambi ya Upinzani.

Mbali na kutangaza mkakati huo Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kuweka mkakati huo imesema kuwa kauli ya Ndugai ni kauli ya udhalilishaji kwa Bunge kwani hakuna maamuzi ya pamoja ambayo yalifanywa na bunge kwa ajili ya kutofanya kazi na CAG.

Kwa niaba ya Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kibamba John Mnyika alisema kuwa kauli ya Spika ya kutangaza kuwa Bunge limeazimia kutofanya kazi na CAG ni nia yake mwenyewe na wala hakuna kamati yoyote ikiwemo kamati ya Uongozi wa Bunge ambayo imekubaliana na jambo hilo.

Mnyika alisema kuwa kamati yaUongozi ya Bunge haijawahi kufanya kikao chochote juu ya kauli aliyoitoa Spika Ndugai na kutokana na hali hiyo taifa na wananchi wanatakiwa kutambua kuwa uamuzi uliofanyika ni uamuzi binafsi wa Ndugai na siyo wa Bunge kwani kambi rasmi ya upinzani  Bungeni haitambui uamuzi huo.

Kiongozi huyo alisema kuwa kama kweli kuna vikao ambavyo vilifanywa na Kamati ya Uongozi ya Bunge Spika Ndugai ajitokeze hadharani na aeleze vikao hivyo vilifanyika lini na wapi huku Mnyika akihoji kuwa Spika Ndugai alikaa vikao na nani.

Mnyika akizungumza kwa niaba ya Kambi ya Upinzani alisema kuwa Kambi rasmi Bungeni inamtaka Spika kuziacha kamati za Kudumu za Bunge za LAAC na PAC ziendelee na kazi badala ya kuziingilia na kuzizuia kufanya vikao kwa madai kuwa haziwezi kufanya kazi kutokana na kuwepo kwa mgogoro kati ya CAG na Bunge.

Mnyika alisema kuwa Siyo kweli kuwa Bunge lina Mgogoro na CAG na kwa kauli ya Spika kudai kuwa kuna mgogoro kati ya Bunge na CAG ni kauli yake na hizo ni dalili za kufanya kamati hizo zisiweze kupata hoja ambazo walitaka CAG kuzipeleka kwenye kamati kutokana na kuwepo na baadhi ya ubadhilifu wa fedha za Umma ambao haukutolewa ufafanuzi ikiwemo matumizi y ash. Trilioni  1.5 ambazo hazijulikani matumizi yake.

“Kwa mujibu wa mgawanyo kamati za Bunge  za Bunge za LAAC na PAC ambazo zinaongozwa na wapinzani zimesitishwa kufanya kazi zake kuanzia januari 14 mpaka januari 25 mwaka huu tafsiri yake kwa mujibu wa ratiba za Bunge iliyotangazwa kamati za Bunge zinamaliza kazi zake kimsingi 25 Januari mwaka huu na 26 na 27 januari ni siku za Mapumziko ili hatimaye kikao cha bunge kiweze kuanza 29 Januari mwaka huu.

“Kwa hiyo kimsingi Spika wa Bunge amesitisha kabisa katika kipindi hiki kamati za Bunge za PAC na LAAC kufanya kazi zao kikatiba za kisheria na kikanuni kwa mujibu wa ratiba jambo ambalo kambi rasmi ya upinzani tunalipinga hatuungi mkono kabisa uamuzi huu wa Spika kuzisambaratisha hizi kamati mbili muhimu na tunamtaka spika wa Bunge abadilishe mara moja huu uamuzi wake ili kamati hizo ziruhusiwe  kukutana kabla ya 25 Januari ziweze kufanya kazi zao za kikatiba,” alieleza Mnyika.

“Ni vyema Umma ujue kuwa 14 Januari kamati ya Bunge ya PAC kwa mujibu wa ratiba ya mwanzo iliyotangazwa na Bunge , ilikuwa inafanya kikao cha pamoja na CAG  ili kupata ufafanuzi juu ya taarifa ya ukaguzi wa hesabu za serikali kuu kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2017.

“Tafsiri yake ni nini, yale mambo yote yaliyoibuliwa na CAG  mwaka 2017 ikiwemo suala la Sh. 1.5 trilioni, CAG alieleza katika taarifa yake kwamba hakuna uwiano kati ya fedha na matumizi ya takribani ya Trilioni 1.5 lakini CAG hakwenda mbali katika taarifa yake kueleza kwa kina hivi hizi fedha ambazo zinatuhumiwa hazijulikani ziko wapi zilitumikaje tumikaje na zilitumika na akina nani.

“Serikali ilitoa maelezo ambayo CAG aliagizwa akayafanyie kazi ili alete taarifa ya kina kuhusu Trilioni  1.5 ziko wapi zimetumikaje ilipaswa januri 14 mwaka CAG atokee mbele ya kamati kuleta ripoti kwa Bunge ili  lifanye uchambuzi na liandae maoni na mapendekezo ambayo kwa ratiba ya Bunge yalipaswa yaingie katika mkutano wa Bunge unaoanza 29 Januari mwaka huu,lakini ili kukwepesha serikali kuwajibika mbele ya Bunge, Spika wa Bunge akaamua kuanzia 14 Januari kusambaratisha kamati ya PAC na LAAC na kutangaza kile alichokiita kwamba ni mgogoro kati ya CAG na Bunge kwa kusema Bunge limesitisha kufanya kazi na CAG kitu ambacho siyo sahihi.

“Napenda kusisitiza sisi kama kambi rasmi ya upinzani hatukubaliani nalo na tunatamka kwamba Spika wa bunge abadilishe uamuzi wake ili kuruhusu kamati za bunge za LAAC na PAC na kamati nyingine kufanya kazi zake kama kawaida na CAG.

“Na kama CAG aliitwa 21 januari ni nini Spika wa Bunge kilimfanya kusitisha hizo kamati kufanya kazi na CAG kwanini asingesubiri kwanza tarehe hiyo ndipo ifanye maamuzi,kitendo cha kusitisha shughuli mpaka 25 tarehe ambayo ndio mwisho wa vikao vya kamati  za bunge kinaashiria kwamba katika mawazo ya Spika tayari ilishafanya uamuzi kabla ya kamati ya Bunge kumshauri kama alivyosema,” alisema Mnyika.

Mbali na hayo Mnyika alisema kuwa kambi rasmi imekuwa ikipata taarifa ya kuwa msimamao wa CAG kutoa hati  chafu katika baadhi ya taasisi kumekuwa tishio kwa serikali na kuhofia kuwa kunaweza kutokea taarifa nyingine mbaya kwa serikali ambazo zilitakiwa kufanyiwa uchunguzi maalum.

Kwa upande wake mbunge wa Momba na Waziri Kivuli wa Wizara ya Fedha na Mipango David Silinde (Chadema) alisema kuwa bunge limekuwa ni bunge la kwanza kupingana na kazi zinazofanywa na CAG.

Silinde alisema kuwa kitendo ambacho kinafanywa na Bunge kwa kupingana na CAG kunaweza kusababisha wahisani kusitisha misaada ambayo wanakusudia kuitoa kutokana na kuwa na mashaka juu ya matumizi ya mashaka ya matumizi ya fedha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Askofu Wolfang Rais mpya TEC, Padri Kitima aula tena

Spread the loveBARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetambulisha safu mpya za...

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yaahidi kushirikiana na Prof. Ndakidemi kuhamasisha zao la kahawa

Spread the loveSerikali imeahidi kuungana na Mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

IMF yaimwagia Tanzania trilioni 2.4 kukabili mabadiliko ya hali ya hewa

Spread the loveShirika la Kimataifa la Fedha (IMF) jana Alhamisi limesema bodi...

error: Content is protected !!