Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kambi ya Maalim Seif yatikiswa
Habari za Siasa

Kambi ya Maalim Seif yatikiswa

Spread the love

KAMBI ya Maalim Seif Shariff Hamad, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) imeendelea kutikiswa na utawala wa Rais John Magufuli baada ya mfuasi wake ambaye ni Mbunge wa Kilwa, Seleman Bungara ‘Bwege’ kukamatwa na kisha kutolewa kwa dhamana jana. Anaandika Faki Sosi … (endelea).

Bwege ambaye amejitenga na kambi ya Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CUF Taifa, alikumbana na dhahama ya kukamatwa na polisi jana kwa madai ya kutaka kufanya mkutoa bila kibali.

“Alikamatwa jana lakini hakulala, alitoka jana ile ile kwa kuwa, kilichokuwa kikitakiwa ni kukamilishi masharti ya dhamana na yalikamiika hivyo alitoka,” ameeleza Mbarara Maharagande, Mkurugenzi Habari na Mawasiliano CUF.

Bwege alikamatwa tarehe 1 Oktoba 2018 kwa tuhuma ya kutoaka kufanya mkutano bila kibali kwenye eneo linalotambulika kwa jina la Maalim Seif lililopo Kilwa Kivinje.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa, Bwege alitekeleza matakwa ya kisheria katika kupeleka barua kuwahabarisha polisi kuhusu mkutano wake, hata hiyo aliambiwa asifanye mkutano huo kwa maelezo kuwa hali ya usalama haipo imara.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!