Tuesday , 3 October 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni, njiapanda
Habari za SiasaTangulizi

Kambi Rasmi ya upinzani Bungeni, njiapanda

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

KAMBI Rasmi ya upinzani bungeni, iko hatarini “kusambaratika” kufuatia “mapinduzi” ya kisiasa, yaliyotokea ndani ya Chama cha Wananchi (CUF). Anaripoti Danson Kaijage kutoka Dodoma … (endelea).

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya wabunge wa CUF zinasema, ni vigumu mno kwa wabunge wa chama hicho, kuendelea kushirikiana na wenzao wa Chadema, katika uendeshaji wa kambi hiyo.

Kambi rasmi ya upinzani bungeni, ilikuwa inaundwa na wabunge kutoka vyama vya NCCR- Mageuzi, chama cha ACT- Wazalendo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na baadhi ya wabunge kutoka CUF.

Uwezekano wa “kusambaratika” kwa kambi hiyo, unatokana na hatua ya mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, kutangaza kutoshirikiana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Kambi Rasmi ya upinzani bungeni, inaongozwa na Freeman Mbowe, mbunge wa Hai (Chadema) na mwenyekiti wa taifa wa chama hicho.

Hata hivyo, mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya wabunge wa CUF, Suleman Bungara (Bwege), ameeleza MwanaHALISI Online kuwa yeye na baadhi ya wenzake, hawaamini katika utengano.

Anasema, “mimi naamini katika umoja. Siamini katika utengano. Nje ya umoja, hatuwezi kushinda jimbo lolote la uchaguzi. Hata pale Kilwa, hatuwezi kushinda kama hatutakuwa na umoja.”

Akizungumzia kauli ya Prof. Lipumba, mbunge huyo wa Kilwa Kusini anasema, “huyo amesema yeye kama yeye na siyo kama taasisi.”

Anaongeza, “…kauli yake haijatokana na vikao vya Baraza Kuu ama Kamati Kuu (Kamati Tendaji), ni kauli yake binafsi. Na mimi naichukulia hivyo. Na kwa msingi huo, mimi binafsi nitaendelea kushirikiana na UKAWA.”

“Kushinda bila kushirikiana hakuwezekani, kama tunataka ushindi ni lazima tushirikiane. Kama Prof. Lipumba alisema hayo, pengine ni kutokana na mgogoro uliyokuwapo. Sisi tutaendeelaa kushirikiana kwa msingi kwamba umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.”

Chama cha CUF, kimekubwa na mgawanyiko mkubwa uliokimega chama hicho mapande mawili, kufuatia Prof. Ibrahim Lipumba, kurejeshwa kwenye uongozi wa chama hicho na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.

Kufuatia maamuzi hayo, aliyekuwa katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, pamoja na wafuasi wake waliamua kwenda mahakamani na baadaye wakatangaza kukihama chama hicho na kujiunga na ACT- Wazalendo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bilioni 6.1 kumaliza tatizo la maji Katoro-Buseresere – Geita

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa Umoja wa wanawake CCM, (UWT), Zainab Shomari...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kupokea ndege ya 14 ya ATCL, safari kuongezeka

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania, kesho tarehe 3 Oktoba 2023, inatarajia...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mobhare Matinyi Msemaji mpya wa Serikali

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa Mkuu wa...

Habari MchanganyikoTangulizi

Basi la Magereza lagonga treni yenye abiria 650 Dar

Spread the loveBasi  Jeshi la Magereza lenye namba MT 0040 limegonga treni...

error: Content is protected !!