Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kambaya kujenga kituo cha biashara, mabasi mbagala
Habari za Siasa

Kambaya kujenga kituo cha biashara, mabasi mbagala

Spread the love

MGOMBEA Ubunge wa Mbagala jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Abdul Kambaya amewaomba wananchi wa jimbo hilo kumpa fursa awatumikie ili kutumia ukuwaji wa makazi na idadi ya wakazi kuwa fursa za kiuchumi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kambaya akihutubia mkutano wa kampeni Kata ya Kiburugwa alisema, atatumia wingi huo wa makazi kama fursa ya kiuchumi kwa kuongeza mzunguko wa fedha ndani ya Jimbo hilo.

Alisema mzunguko mdogo wa fedha na ukata wa kimaisha unaweza kupungua kwa kuanzisha Kituo cha Biashara Mbagala.

“Kituo hiki, kitajengwa Mbagala Zakiem na kitakusanya bidhaa zote muhimu za majumbani na maofisini ikiwemo mavazi, vifaa vya ujenzi na vipuri vya vya magari na pikipiki,” alisema Kambaya

Alisema wafanyabiashara wakubwa na wadogo watapewa nafasi kwa ajili ya kusambaza bidhaa zao.

Kambaya alisema, jambo hilo litaongeza mzunguko wa fedha kwakuwa wanunuzi wanakwenda Kariakoo wakitokea Mbagala au mikoa ya Tuhuma kwa maana ya Tunduru na mikoa ya Mtwara na Lindi hawatakuwa na sababu ya lazima ya kwenda Kariakoo kufunga mzigo na badala yake watapata bidhaa hizo Kituo cha Biashara Mbagala.

Ahadi nyingine, Kambaya ameahidi kujenga au kuanzisha Kituo cha Mabasi ya mikoa ya Kusini ya Mtwara na Lindi ili kuondosha kero ya kuanzia safari zao Kituo cha Ubungo.

“Kituo hiki kitarahisisha ukuwaji wa Kituo cha Biashara Mbagala kwa maana ya kutuletea wanunuzi toka mikoa ya Kusini na kwa hali hiyo, wafanyabiashara wa nyumba za kulala wageni na hata wafanyabiashara wa vyakula watapa wateja,” amesema Kambaya

Pia amesema, itarahisisha usafiri wa bidhaa za wanunuzi watokao mikoa ya kusini.

Kambaya alisema, ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Biashara utatekelezwa kwa kutumia fedha za mfuko wa Jimbo ambazo ni takribam Sh.1.5 bilioni kwa maana ya Sh.300 milioni kila mwaka na misaada ya mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya Tanzania.

“Nitapeleka pendekezo kwa madiwani wa Jimbo la Mbagala kuweza kubariki fedha hizi ziweze kutumika kwenye mradi huu kwa kuwa utakuwa na manufaa kwa Jimbo la Mbagala kwa kuongeza mzunguko wa fedha na kulegeza vyuma vilivyokaza,” alisema

“Kituo cha Mabasi kwa kuwa hakina gharama kubwa kitajengwa kwa mapato ya ndani ya Manispaa ya Temeke. Uboreshwaji wa huduma za Jamii kama vile elimu, afya, miundombinu utafanyika kwa kutumia bajeti za wizara husika,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!