Thursday , 25 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kamati ya kufufua mchakato wa Katiba mbioni kutangazwa
Habari za Siasa

Kamati ya kufufua mchakato wa Katiba mbioni kutangazwa

Rais Jakaya Kikwete (kushoto) na Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein (katikati) wakionesha katiba Mpya
Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema hivi karibuni Serikali yake itatangaza kamati itakayokuwa na jukumu la kusimamia ufufuaji mchakato wa marekebisho ya katiba, uliokwama tangu 2014. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Mkuu huyo wa nchi ametoa ahadi hiyo leo tarehe 8 Machi 2023, katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro, baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kumuomba marekebisho hayo yakamilike kabla 2025.

“Nilikuwa nasema hivi, suala la katiba hakuna anayelikataa hata chama changu kimesema twende kwenye mabadiliko ya katiba, hakuna anayelikataa lakini mdogo wangu Aikael kasema juzi leo lifanyike, mambo ni mengi ndani ya nchi lakini niwaahidi si muda mrefu tutatangaza hiyo kamati kwa kushirikiana na vyama vya siasa ili waende wakaanze kazi,” amesema Rais Samia.

Katika hatua nyingine, Rais Samia ametumia madhimisho yaliyoandaliwa na Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), kuwataka wananchi bila kujali tofauti zao za itikadi za kisiasa na dini, kukomesha vitendo vya mmomonyoko wa maadili nchini.

“Suala la maadili ya vijana wetu haipendezi, haifurahishi na hakuna wa kumtupia lawama. Lawama ni kwamba jamii yetu ya Tanzania tulitetereka kwenye malezi na dini. Twendeni tukaangalie tulikokosea, wapi tulinde mila na desturi yetu. Kuna mengine ya kuletewa tukatae,” amesema Rais Samia.

Kuhusu haki za wanawake, Rais Samia amewataka wanawake wa Bawacha washirikiane na wanawake kutoka vyama vingine vya siasa, kupigania maslahi ya kundi hilo.

“Ile nguvu ya watu ya wanawake wa Chadema ikaunganishe kila chama tukamkomboe mwanamke wa Tanzania, tukakuze uchumi ili yale tunayolilia hapa yakatekelezwe. Mkianza kuweka mipaka sitafanya na yule sababu hana hili hana hili hatutafika,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!