Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Kamati ya kitaifa kuratibu matumizi mabaya mitandaoni yaundwa
Habari Mchanganyiko

Kamati ya kitaifa kuratibu matumizi mabaya mitandaoni yaundwa

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imeunda kamati ya Taifa ya kusimamia utatuzi wa matumizi mabaya ya huduma na bidhaa za mawasiliano. Anaripoti Noela Shila, TUDARCo…(endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi, tarehe 9 Septemba 2021 na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew wakati akijibu swali la Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Emmanuel Mwakasaka.

Mwakasaka ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya haki, maadili na madaraka ya Bunge ameuliza serikali ina mikakati gani ya ziada ya kudhibitisha tatizo la utapeli na wizi wa kimtandao kupitia simu za mikononi.

Akijibu swali hilo, Mhandisi Mathew amesema, mwaka 2015 serikali ilitunga sheria ya makosa ya mitandao kwa lengo la kutambua kisheria makosa yanayofanyika kwenye mitandoa ili kuweza kuchukua hatua stahiki yanapobainika makosa hayo.

Pia, ilitungwa sheria ya miamala ya kielekroniki kwa lengo la kutambua miamala inayofanyika kimtandao.

Mhandisi Mathew amesema, Serikali ilianzisha kitengo cha uhalifu wa mitandao chini ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa makosa ya mitandao ikiwemo wizi wa aina yoyote kwenye mtandao na kuandaa majalada ya kufungulia mashtaka kwa kusaidiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

“Watuhumiwa wanaokamatwa kutokana na matumizi mabaya ya mitandao huchukuliwa hatua stahiki,” amesema

Naibu waziri huyo amesema, Februari 2021 serikali ilihusisha wizara na taasisi zinazojihusisha na makosa ya mitandao kuweza kutatua maswala yanayoyakabili mitandao pamoja na wizi unaoendela mitandaoni.

Pia amesema serikali kwa kushirikiana na watoa huduma za simu za mkononi imeanzisha mfumo kupitia namba “15040” wa kupokea na kuzifungia namba ambazo zimeripotiwa na kuthinitika kutuma ujumbe au kupiga simu za utapeli.

Amesema, baada ya kuthibitisha namba hizo kufanya vitendo hivyo, namba husika hufungiwa, kitambulisho cha NIDA kilichotumiwa kusajili namba husika kufunguwa kusajili na kifaa kilichotumika (simu) pia kufungiwa ili kisifanye kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!